Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi maeneo ya Vituo vya afya-Infection Prevention and Control (IPC)
Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi maeneo ya Vituo vya afya-Infection Prevention and Control (IPC).
Je IPC inazingatiwa kwenye hospital,Vituo vya afya,Zahati,maabara n.k?
Swala la Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi maeneo ya Vituo vya afya yaani “Infection Prevention and Control (IPC)” ni muhimu sana ili kuzuia kuenea kwa magonjwa mbali mbali,
Njia za Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi ya magonjwa mbali mbali maeneo ya Vituo vya afya-Infection Prevention and Control (IPC) ni pamoja na;
- Kuzingatia sana Swala la usafi wa mikono(hand hygiene),
- kufanya uchunguzi wa mapema(early screening)
- Pamoja na kutengwa kwa mgonjwa(patient isolation)
Vyote hivi ni muhimu sana katika kuzuia kuenea kwa magonjwa. ✅
Pia Janga la Korona(COVID19) limetoa fursa ya kipekee ya kuboresha IPC kote;kwenye maeneo mbali mbali,
Janga hili limeonyesha umuhimu mkubwa wa kuzingatia “IPC” kwenye kila eneo.
NB: Kama ni mfanyakazi wa afya hakikisha unazingatia sana na kufuata kanuni zote za “IPC” ili Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kwa wagonjwa wako pamoja na wafanyakazi wenzako.