Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mloganzila:Idadi ya wagonjwa wa kuchuja damu imeongezeka kutoka wagonjwa 91 hadi 157

Idadi ya wagonjwa wa huduma za kuchuja damu imeongezeka kutoka wagonjwa 91 hadi kufikia wagonjwa 157-Mloganzila.

Kutokana na maboresho ya huduma pamoja na huduma bora kwa wateja katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila, idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa huduma za kuchuja damu imeongezeka kutoka wagonjwa 91 kwa kipindi cha Januari-Machi 2022 na kufikia wagonjwa 157 kwa kipindi kama hicho mwaka 2023 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 72.

Hatua hiyo inatokana na maboresho makubwa yaliyofanywa katika sekta ya afya na Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza vifaa tiba na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo MNH-Mloganzila Dkt. Immaculate Goima amesema uelewa wa dalili za magonjwa yasiyo ya kuambukiza miongoni mwa jamii umeongezeka jambo ambalo limepelekea wagonjwa kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na kuanza matibabu mapema.

Dkt. Goima ameongeza kuwa Mloganzila imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa jamii ya namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza .

Akizungumzia kuhusu huduma za kupandikiza figo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo MNH-Mloganzila Gyunda Anthony amesema Mloganzila ilifanya upandikizaji kwa wagonjwa watatu ambapo kumekuwa na mafanikio kwani wagonjwa hao na ndugu waliowachangia figo wanaendelea vizuri na kufanya shughuli zao kama kawaida.

“Wagonjwa hawa tuliowapandikiza figo , wanakuja kliniki kwa ufuatiliaji wa afya zao mara moja kwa mwezi , kabla ya kupandikizwa figo walikua wanafanya dialysis mara tatu kwa wiki na kukaa zaidi ya saa nne kwenye mashine ya kuchuja damu kila walipohudhuria hospitali kwa ajili ya huduma hiyo “ amefaafnua Dkt. Gyunda.

Ameishauri jamii kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kufanya mazoezi, kuzingatia ulaji sahihi kwa kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga na sukari na pia kula matunda na mboga mboga kwa wingi ili kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza.

@muhimbili_mloganzila

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.