Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mtoto huanza kukojoa baada ya Muda gani toka azaliwe? Fahamu hapa

Mtoto huanza kukojoa baada ya Muda gani toka azaliwe? Fahamu hapa

Wapo wazazi ambao wamekuwa na wasiwasi kuhusu swala la watoto wao kutokukojoa toka wazaliwe, je hii ipoje?

Watoto wachanga wanaonyonyeshwa kiwango cha kukojoa hubadilika kila siku katika wiki ya kwanza toka wazaliwe,

Katika siku chache za kwanza, mtoto wako mchanga anaweza asipate maziwa mengi kutoka kwako hali ambayo huweza kumpelekea kutokukojoa mara nyingi.

Kisha, kadiri siku zinavyosonga mbele na kiwango cha kupata maziwa ya mama wakati ananyonyeshwa huongezeka, hii pia itapelekea mtoto wako kutoa mkojo mwingi zaidi.

Tunatarajia mambo haya kutokea kwa mtoto anayenyonyeshwa maziwa ya mama;

1. Siku ya kwanza(Day 1):

Mtoto mchanga atatokwa na mkojo kwa mara ya kwanza ndani ya masaa 12 hadi 24 baada ya kuzaliwa.

Wakati wa saa za mwanzoni na siku za kwanza baada ya mtoto kuzaliwa, mtoto anayenyonyeshwa maziwa ya mama pekee anaweza asikojoe mara nyingi sana.

2. Siku ya pili(Day 2):

Mtoto mchanga anatakiwa kukojoa angalau mara mbili kwa siku hadi matiti yako yaanze kujaa maziwa kwa siku ya tatu au ya nne baada ya kujifungua;

kadiri mtoto anavyonyonya maziwa Zaidi, ndivyo kiwango cha Mkojo au kukojoa huongezeka.

3. Siku ya tatu mpaka ya tano(Days 3–5):

Mtoto wako anatakiwa kukojoa angalau mara 3 mpaka 5 kwa siku.

4. Siku ya Sita na kuendelea(Day 6) and on:

Mtoto wako anatakiwa kukojoa angalau Mara sita mpaka nane kwa siku(kila masaa 24), Ingawa pia baadhi ya watoto hukojoa zaidi hata kila baada ya kunyonya.

Tunatarajia mambo haya kutokea kwa mtoto anayepewa Maziwa ya Kopo(Bottle-Fed Infants);

Kiasi cha mkojo ambacho mtoto wako mchanga hutoa kinahusiana moja kwa moja na kiasi cha maziwa anachopewa,

Ikiwa mtoto wako ni mlaji mzuri utaona anakojoa zaidi. Lakini, ikiwa mtoto wako mchanga hapati kiwango cha kutosha cha maziwa, atakuwa anakojoa mara chache zaidi.

kwa mtoto mchanga anayelishwa vizuri:

  1. Siku ya kwanza(Day 1):Mtoto anapaswa kuanza kukojoa saa 12 hadi 24 toka azaliwe.
  2. Siku ya pili(Day 2): Mtoto anatakiwa kukojoa angalau mara mbili kwa siku
  3. Siku ya tatu mpaka ya tano(Days 3–5): Mtoto anatakiwa kukojoa angalau mara tatu mpaka tano kwa siku
  4. Siku ya Sita na kuendelea(Day 6 and on): Mtoto anatakiwa kukojoa angalau mara sita mpaka nane kwa siku.

Kumbuka; Kukojoa Baada ya Wiki ya Kwanza toka mtoto azaliwe Iwe unampa maziwa ya chupa au unanyonyesha, Unapaswa kuona angalau mtoto anakojoa mara sita hadi nane kila siku,lakini mtoto wako anaweza kukojoa hata hadi mara 10 au zaidi kulingana na kiwango cha maziwa anachopata.

Onana na Wataalam wa afya endapo;

– Mtoto anakojoa sizaidi ya mara sita kila siku baada ya siku ya tano toka azaliwe.

– Mtoto anakojoa kiasi kidogo sana cha mkojo mweusi sana, wa manjano, uliokolea, na unaonuka baada ya siku ya nne.

– Mtoto ana usingizi usio wa kawaida na ni vigumu kuamka.

– Mdomo wa mtoto pamoja na Lips zake ni kavu sana

– Mtoto kupumua kwa shida

– Mtoto kutokunyonya

– Kuona damu kwenye Mkojo wa Mtoto mchanga, Ukiona damu yoyote kwenye mkojo wa mtoto wako halafu mtoto analia au anaonyesha dalili za kukojoa kwa maumivu, wasiliana na daktari wa mtoto wako mara moja.

– Mtoto kutokukojoa kabsa, Kama Mtoto mchanga hakojoi mkojo mwingi anapaswa kukojoa angalau mara mbili kwenye siku chache za kwanza unapotengeneza kolostramu.

Lakini, mtoto wako anapofikisha umri wa siku sita, anapaswa kukojoa mara sita kwa siku. Ikiwa mtoto wako hakojoi mkojo wa kutosha au hana mkojo kabisa, Wasiliana na daktari mara moja.

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.