Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la mama Mjamzito kupitisha muda wa Kujifungua(POSTTERM PREGNANCY)

Tatizo la mama Mjamzito kupitisha muda wa Kujifungua(POSTTERM PREGNANCY)

Tatizo la mama mjamzito kupitisha muda wa Kujifungua yaani Postterm Pregnancy linatokea pale ambapo Mimba imekaa baada ya wiki 42 za ujauzito,

ambapo umevuka muda wa kawaida wa mama Kujifungua (wiki 37-40-42). Hali ya ujauzito kupitisha Muda wake huweza kuleta hatari kwa mama na mtoto, kama vile kusababisha;

  • Tatizo la Utapiamlo kwa mtoto(fetus)
  • Mama kupoteza maisha
  • Magonjwa yanayotokana na mtoto kunywa meconium
  • Na kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa. Kumbuka Baada ya wiki ya 42 ya ujauzito, kondo la nyuma, ambalo humpa mtoto virutubisho na oksijeni kutoka kwa mama, huanza kuzeeka na mwisho kushindwa kufanya Kazi hiyo.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA MAMA KUCHELEWA KUJIFUNGUA(POST TERM PREGNANCY)

Sababu za moja kwa moja zinazosababisha mwanamke kupitisha mda sahihi wa Kujifungua hazijulikani. Lakini sababu zinazochangia hali hii ni pamoja na;

– Mama kuwa na Historia ya Kuchelewa au kupitisha Mda wa Kujifungua katika Ujauzito Uliopita(History of postterm delivery from Previously Pregnancies)

– Mama kuwa na tatizo la Uzito kupita kiasi au Unene(Maternal Obesity)

– Matatizo katika Mfumo mzima wa fahamu

– Upungufu wa kiwango cha Sulphur kwenye placenta au kondo la Nyuma

– Tatizo linalohusu mtoto kuwa na shida kwenye kichwa kama vile Anecephaly

-Tarehe za matarajio(Expected date of Delivery- EDD) kwa mama Kujifungua kukosewa wakati mama akiwa hakumbuki vizuri kuhusu hedhi yake ya mwisho.  Hii huweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya Mda uliotarajiwa au kupitisha mda uliotarajiwa mama Kujifungua

Kwahyo ni Muhimu sana mwanamke kufanyiwa Ultrasound ili kupata Majibu sahihi juu ya Tarehe hizi.

– Tafiti zinaonyesha pia mwanamke mwenye matizo katika Mzunguko wake wa hedhi kabla ya kupata mimba pamoja na Matatizo ya hormones huweza kupatwa na tatizo hili

?DALILI ZA MWANAMKE KUPATA TATIZO LA KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POST TERM DELIVERY)

➖ Kwa sababu tatizo hili la mwanamke kupitisha mda sahihi wa kujifungua linategemea tu umri wa ujauzito, hakuna dalili za mwili zinazothibitisha uwepo wa tatizo hili.  Dalili za kawaida zinazoweza kuashiria uwepo wa hali hii ni pamoja na;

  1.  ngozi ya mwili kuwa kavu
  2. Uwepo wa mikunjo kwenye mitende ya mtoto na nyayo za miguu yao baada ya kuzaliwa
  3. Mtoto kuzaliwa na nywele nyingi kichwani, na ngozi ya kahawia, kijani kibichi, au manjano. N.k

MATIBABU

-Yapo matibabu mbali mbali kama Vile,Mama kupewa dawa ya Kuanzisha uchangu pamoja na Kuongeza uchungu ili Ajifungue kwa haraka.

– Au pia mama Kufanyiwa Upasuaji na mtoto kutolewa  Nje.

Kumbuka; Mahudhurio ya Kliniki kwa Mama Mjamzito ni muhimu sana kwani ndyo huchangia kuleta uzazi salama kwa asilimia 99% Hasa kwa mwanamke au mama ambaye hupata matatizo kipindi cha Ujauzito

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.