Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ugonjwa wa Kaswende husababisha zaidi ya Vifo 300,000 vya watoto waliotumboni na watoto wachanga kila mwaka Duniani

Ugonjwa wa Kaswende husababisha zaidi ya Vifo 300,000 vya watoto waliotumboni na watoto wachanga kila mwaka Duniani.

Fahamu kwamba kwa Mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO);

Duniani kote,Ugonjwa wa Kaswende kwa Wajawazito husababisha zaidi ya Vifo 300,000 vya watoto waliotumboni na watoto wachanga kila mwaka,

Kaswende ni maambukizi ya bakteria yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana, au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua.

Ugonjwa huu ukiachwa bila kutibiwa, unaweza kusababisha matatizo makubwa na hata kutishia maisha,

Ugonjwa wa Kaswende kwa mama mjamzito unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo;

  • Mimba kutoka zenyewe(miscarriage)
  • Kuzaa mtoto akiwa amefariki(stillbirth)
  • Kuzaa mtoto mapema kabla ya wakati au kuzaa mtoto Njiti(premature birth)
  • Au kusababisha udumavu kwenye ukuaji wa mtoto tumboni(fetal growth restriction)

NB:Kama ni Mjamzito; Hakikisha unapimwa ugonjwa wa kaswende na endapo umepatikana una ugonjwa huu hakikisha unapata Tiba Mapema Zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.