Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Upasuaji wa kwanza wa Ukarabati wa Mrija wa Mkojo wafanyika,Hospital ya LIGULA

Upasuaji wa kwanza wa Ukarabati wa Mrija wa Mkojo wafanyika,Hospital ya LIGULA

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara-Ligula kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji wa ukarabati wa mrija wa mkojo (Urethroplasty) kwa kuchukua nyama sehemu ya mdomo kwa mgonjwa na kuipandikiza kwenye sehemu ya mrija wa mkojo kwa mgonjwa ambae alionekana na tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo.

Upasuji huo umefanywa na Madaktari Bingwa wakishirikiana na Madaktari wa Hospitali hiyo wakati wa kambi maalumu ya madaktari hao (Madaktari Bingwa wa Mama Samia)

Upasuaji na ukarabati wa mrija na mkojo umefanyika baada ya uchunguzi wa mionzi kutoka kambi maalumu ya Madaktari Bingwa kufanyika katika Mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Mtwara.

Akizungumza baada ya kukamilisha upasuaji huo Daktari bingwa bobezi wa mfumo wa mkojo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Dkt. Hussein Msuma amesema upasuaji huo umefanikiwa kufanyika kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo kwa gharama nafuu na kumpunguzia mgonjwa gharama za kusafiri kufuata huduma hiyo Jijini Dar es salaam.

“Upasuaji huu umempunguzia gharama kubwa baada ya kuja kuhudhuria hapa katika kambi hii maalumu ya uboreshaji wa huduma za afya nchini ambayo ni kambi ya madaktari bingwa wa Mama Samia”. Amesema Dkt. Msuma

Katika kambi hiyo madakatari hao bingwa na bobezi wameweza kuwajengea uwezo madaktari wa ndani ya hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara – Ligula ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa mkojo kuanzia hatua ya kuwaona katika kliniki za upasuaji hadi kuwafanyia upasuaji.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.