Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Vyakula ambavyo ni chanzo kizuri cha Maji

Vyakula ambavyo ni chanzo kizuri cha Maji

Kunywa Maji sio njia pekee ya kuongeza maji mwilini, Kwa kawaida unaweza kupata karibu asilimia 20% ya maji kila siku kutoka kwenye chakula.

Unaweza kupata hata zaidi ikiwa unakula vitu fulani. Na kuna faida za kuongeza maji kupitia chakula, Hii husaidia mwili kufyonza maji polepole zaidi na kupata virutubisho pia.

Vyakula ambavyo ni chanzo kizuri cha Maji

Hapa tunazungumzia vyanzo vingine vya maji mwilini mbali na kunywa maji yenyewe, Hivo basi, kuna vyakula mbali mbali ikiwemo matunda na mboga ambavyo vitakusaidia wewe kuongeza maji mwilini kwa kiasi kikubwa,

Hivi hapa ni baadhi ya vyakula ambavyo ni chanzo kizuri cha Maji;

1. Matango

Matango yana asilimia 95% ya maji na kiwango kidogo cha kalori, Matango pia yanaweza kusaidia kupambana na kuvimba(Inflammation) kwa aina mbali mbali na hata kupunguza mchakato wa kuzeeka.

2. Carrots

Hii  inaweza kukushangaza, kwa hali ya kawaida huwezi kufikiri kuwa Karoti inaweza kuchangia kuongeza maji mwilini.

Lakini pia tafiti zinaonyesha karoti ina karibu asilimia 90% za maji, Na beta carotene pamoja na antioxidants zinazoweza kukulinda dhidi ya saratani na kuimarisha afya ya moyo.

3. Spinach

Spinach ni mboga ya majani ambayo inaweza kutumika mbichi kwenye saladi au kupikwa.

Haina maji mengi sana lakini huweza kuchangia kiasi flani cha maji mwilini na pia imesheheni virutubisho kama vile;

  • vitamini K,
  • folate,
  • manganese
  • magnesiamu,
  • pamoja na vioksidishaji au antioxidants zinazosaidia kupambana na uvimbe pamoja na saratani mwilini.

4. Supu na Mchuzi

Utengenezaji wa supu kwa kiasi kikubwa huhusisha kiwango kikubwa cha vimiminika au liquid.

Hivo unywaji wa Supu huweza kuongeza kiwango kikubwa cha maji mwilini Lakini pia ni njia nzuri ya kupata nyuzinyuzi na virutubisho vingine.

Unaweza kutengeneza Supu mbali mbali ikiwemo;

  • Supu ya Kuku
  • Supu ya nyama ya ng’ombe n.k

Supu ya kuku ya kujitengenezea sio tu nzuri kwa kuongeza maji, lakini pia inaweza kusaidia kupambana na homa ya kawaida au Mafua.

Pia mchuzi huweza kuongeza maji mwilini kwani kiasi kikubwa cha mchuzi ni vimimika(liquid),

Tengeneza mchuzi kutoka kwa samaki, kuku, au mboga, na uongeze karibu kila kitu,

Unaweza kupata mchuzi kutoka kwa maharage hadi mboga mboga na nyama pia.

5. Nyanya

Nyanya zina asilimia 95% ya maji, na zinaweza kuongeza ladha na utamu kwa chakula.

Pia nyanya zina antioxidants nyingi ikiwemo lycopene ambayo inaweza kusaidia kupambana na saratani.

Nyanya zinaweza pia kusaidia kupunguza cholesterol “mbaya” (LDL) na inaweza kuboresha afya ya moyo wako kwa ujumla.

6.Tikiti maji

Tikiti maji ni chanzo kizuri sana cha kuongeza Maji mwilini, tunda la Tikiti maji lina asilimia 91% ya Maji na linaweza kukata Kiu yako,

Ni tamu, lakini lina kiwango kidogo cha kalori, Kama ilivyo kwa nyanya, tunda la tikiti maji lina lycopene nyingi, antioxidant ambayo inaweza kulinda seli zako kutokana na uharibifu wa jua na kusaidia kutunza ngozi  yako.

7. Strawberries

Strawberries pia zina kiwango kikubwa cha maji, zina asilimia 91% ya maji na pia zina antioxidants nyingi, hasa flavonoids — kemikali zinazosaidia ubongo wako kuwa sharp na wenye afya.

8. Yogurt

Yogurt  ina asilimia 85% ya maji, pia ni chanzo kikubwa cha protini na elektroliti ambazo hufanya moyo wako na viungo vingine kufanya kazi inavyopaswa.

Pia ina bacteria (probiotics) ambao ni wazuri kwa usagaji chakula na kusaidia kukuweka sawa.

9. Zabibu

Zabibu zina asilimia 90% ya maji, Hii itasaidia kuongeza kiwango cha maji mwilini.

Pia Zabibu zimejaa nyuzinyuzi(fibers) na virutubisho, hasa vitamini C, ambavyo husaidia mfumo wako wa kinga na inaweza kulinda seli zako dhidi ya uharibifu.

Hitimisho

Hivo ndyo baadhi ya vyakula ikiwemo matunda na mboga,ambavyo ni vyanzo vizuri vya kuongeza maji mwilini mwako.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.