Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Waziri Ummy amepongeza juhudi na mchango wa USAID katika mapambano dhidi ya UVIKO 19

WAZIRI UMMY AAGANA NA BI. VEERAYA (KATE) WA USAID

Na. WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu mapema leo ameagana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Misheni USAID Bi. Veeraya (Kate) Somvongsiri ambaye amemaliza muda wake hapa nchini.

Waziri Ummy amemshukuru Kate pamoja na Serikali ya Marekani kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa Sekta ya Afya nchini kupitia kwa watu wa marekani (USAID).

Aidha, Waziri Ummy amepongeza juhudi na mchango wa USAID katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo kupitia msaada huo Tanzania ilinufaika na msaada wa Dolla Milioni 25 zilizofanikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Bi. Kate ameshukuru kwa ushirikiano ambao Serikali ya Tanzania imekuwa ikiutoa kwa USAID katika kufanikisha malengo ya pamoja ya kuboresha Sekta ya Afya nchini.

“Nashukuru kwa ushirikiano mlionipa katika kipindi chote cha miaka 6 ambacho nilikua nchini hapa toka nikiwa mtumishi wa kawaida USAID hadi kufikia nafasi ya Ukurugenzi” amesema Bi. Kate.

Amesema licha ya kuondoka kwake, USAID itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wake wa Sekta ya Afya katika kuboresha huduma za afya nchini.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.