Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Afya ya moyo:Je, unajua moyo wako hudunda mara 100,000 kwa siku?

Afya ya moyo:Je, unajua moyo wako hudunda mara 100,000 kwa siku?

(Heart beats) Je, unajua moyo wako hupiga/kudunda (kutanuka na kusinyaa) mara 100,000 kwa siku, ukisukuma lita 5 au 6 za damu kila dakika, au takriban galoni 2,000 kwa siku?

Moyo wako ni kiungo cha ajabu ambacho huendelea kusukuma oksijeni na damu yenye virutubisho vingi katika mwili wako ili kuendeleza maisha.

Nguvu hii ya ukubwa wa ngumi hupiga (kutanuka na kusinyaa) mara 100,000 kwa siku, ikisukuma lita 5 au 6 za damu kila dakika, au takriban galoni 2,000 kwa siku.

Moyo wako umetengenezwa kwa misuli(muscles),Wakati kuta za misuli yenye nguvu zinaposinyaa(contract/squeeze)husukuma damu kwenye mishipa ya arteries.

Moyo unapodunda, husukuma damu kupitia mfumo wa mishipa ya damu, unaoitwa circulatory system.

Mishipa hii ipo kwenye mfumo wa elastic ambapo husafirisha damu kwenda kwenye kila sehemu ya mwili.

Damu ni muhimu, Mbali na kubeba oksijeni safi kutoka kwenye mapafu na virutubisho hadi kwenye tishu za mwili wako, pia inachukua taka mwili, ikiwa ni pamoja na carbon dioxide kutoka kwenye tishu. Hii ni muhimu sana ili kudumisha maisha na kuboresha afya ya tishu zote za mwili.

Kuna aina kuu tatu za mishipa ya damu:

(1) Arteries. Hii huanza na aorta, mshipa mkubwa unaotoka moyoni, Mishipa ya arteries hubeba damu yenye oksijeni kutoka kwenye moyo hadi kwenye tishu zote za mwili. Mishipa hii huwa na matawi  kadhaa, ambapo hugawanywika na kuwa vimishipa vidogo vidogo ili kubeba damu mbali zaidi na moyo.

(2) Capillaries. Hizi ni mishipa midogo na myembamba ya damu inayounganisha mishipa ya arteries na the veins.

Kuta zao nyembamba huruhusu oksijeni, virutubisho, kaboni dioksidi, na uchafu mwingine kupita na kutoka kwenye seli za kiungo hiki.

(3) Veins. Hizi ni mishipa ya damu ambayo huchukua damu nyuma ya moyo; damu hii haina oksijeni na ina wingi wa takataka ambazo zinapaswa kutolewa au kuondolewa kutoka kwenye mwili.

Mishipa hii huwa mikubwa zaidi inapokaribia kwenye moyo, Superior vena cava ni mshipa mkubwa ambao huleta damu kutoka kwenye kichwa na mikononi hadi kwenye moyo, na inferior vena cava ambapo huleta damu kutoka kwenye tumbo na miguu kwenda kwenye moyo.

Chemba za Moyo

Moyo ni kiungo chenye vyumba vinne, vyumba hivi Vimegawanywa katika pande mbili(upande wa kushoto na kulia,kisha kutenganishwa na ukuta unaoitwa septum).

Pande za kulia na za kushoto za moyo zimegawanywa zaidi katika vyumba viwili vya juu vinavyoitwa atria, ambayo hupokea damu kutoka kwenye mishipa ya Veins, na vyumba viwili vya chini vinavyoitwa ventricles, ambavyo vinasukuma damu kwenda kwenye mishipa ya Arteries.

Atria na ventrikali hufanya kazi pamoja, husinyaa na kutanuka ili kusukuma damu kutoka kwenye moyo. Damu inapotoka katika kila chemba ya moyo, inapita kupitia kwenye valvu.

Valvu za Moyo

Kuna vali nne ndani ya moyo ambazo ni:

  1. Mitral valve
  2. Tricuspid valve
  3. Aortic valve
  4. Pulmonic valve (au pulmonary valve)

Vali za tricuspid na mitral ziko kati ya atria na ventrikali. Vali za aorta na pulmonic ziko kati ya ventrikali na mishipa mikuu ya damu inayotoka moyoni.

Vali za moyo hufanya kazi sawa na vali za njia moja katika mabomba ya nyumba yako. Zinazuia damu kutoka kwa mwelekeo mbaya.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.