Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Faragha ya mgonjwa ni moja kati ya sheria kuu chache za taaluma ya afya:Waziri wa Afya Mhe.Ummymwalimu

Faragha ya mgonjwa ni moja kati ya sheria kuu chache za taaluma ya afya:Waziri wa Afya Mhe.Ummymwalimu

Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amemuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu kushughulikia maadili ya kitabibu kwa madaktari wanaokiuka taratibu za kitabibu na kutoa taarifa za faragha za wagonjwa hadharani.

Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo kufuatia taarifa  iliyotolewa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa Sokoine Lindi, Dkt. Baraka Steven kuzungumzia faragha ya mgonjwa kinyume na maadili ya kitabibu ambayo inaelekeza taarifa za mgonjwa ni siri.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na mtandao wa EATV, wadau mbalimbali waliibuka na kujadili iwapo ni sahihi kwa daktari kuzungumza na vyombo vya habari kuelezea faragha za mgonjwa bila ridhaa yake.

“Faragha ya mgonjwa ni moja kati ya sheria kuu chache za taaluma ya afya, hapa tuna taarifa zote za mgonjwa kuanzia jina, umri, jinsi yake, makazi na ugonjwa wake, tumeweka taarifa zake za siri kuwa taairfa ya habari” alihoji Bwana Sales Nicco ( @OnlineDentistTz )

“Upo sawa, hii ni kinyume na ethics za kitabibu. Namuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali kulifuatilia na kunipatia Taarifa” amesema Waziri @ummymwalimu akimjibu Bwana Nicco.

Credits:WizaraafyaTz

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.