Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Hospitali chini ya uchunguzi kuhusu madai ya panya kula maiti ya mtoto mchanga:UGANDA

“Sidhani panya wanaweza kufikia maiti ambazo zimehifadhiwa kwenye friji katika chumba cha kuhifadhia maiti [kwa sababu] miili inayopelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti inatibiwa na hainuki.

Iwapo kuna jambo lingine lililoupata mwili wa mtoto huyu, wazazi wanastahili kujua,”  Dk Herbert Luswata, rais wa Chama cha Madaktari Uganda, ambaye hapo awali alifanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Kawempe.

Polisi nchini Uganda wanachunguza Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Kawempe baada ya wanandoa kuhoji hali ya kifo cha mtoto wao mchanga ambaye uso wake daktari katika kituo hicho aliripotiwa kusema kuwa “uliliwa” na panya.

Wazazi hao, Yvonne Ainembabazi mwenye umri wa miaka 20 na mumewe Sulaiman Waiswa, 30, wanadai kuwa mtoto wao wa kwanza huenda alikuwa mwathirika wa kutolewa kafara(ritual sacrifice) na jeraha kubwa upande wa kushoto wa uso lilikuwa haliendani na kuumwa na panya.

Waliambia shirika la kutekeleza sheria kwamba wahudumu wa afya ambao hawakutajwa majina katika hospitali hiyo walipowasili Julai 20 walijaribu kuwapa rufaa “mahali pengine”, wakidai kuwa mtoto wao alihitaji huduma za nje ambazo hazijatajwa, lakini walipinga.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.