Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Huduma ya Kwanza baada ya Kuumwa na NYOKA

Huduma ya Kwanza baada ya Kuumwa na NYOKA

Unapoumwa na nyoka, epuka kugusa sehemu ya jeraha na pia usioshe, kukwangua,

kuchanja au kunyonya sehemu ya jeraha kwani inaweza kusababisha maambukizi au hata sumu ya nyoka kuenea kwa haraka mwilini.

Aidha, kukwangua au kuchanja sehemu ya jeraha inaweza kusababisha damu kutoka bila kukoma endapo utakuwa umeumwa na nyoka wenye sumu inayosababisha damu isigande.

Vilevile epuka kufunga kamba kuzunguka jeraha kwani inaweza kuzuia damu kupita na kusababisha kiungo husika kukatwa.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapata matibabu kutoka katika kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe.

Endapo itatotokea wewe au mtu mwingine ameumwa na nyoka, tulia au mtulize aliyeumwa na nyoka.

Usishtuke, epuka kuwa na papara na wala usikimbie kwani uoga, hofu au kukimbia huongeza kasi ya mapigo ya moyo na hivyo kueneza sumu kwa haraka mwilini.

Vilevile hakikisha kiungo chenye jeraha kisitikisike kwasababu mtikisiko au kukanyagia mguu wenye jeraha husababisha sumu kusambaa kwa haraka zaidi mwilini.

Mgonjwa anatakiwa abebwe au kusafirishwa kwenye vyombo vya usafiri.

Unapoumwa na nyoka, ondoka eneo alipo nyoka, na wala usijaribu kumfuata, kumshika, kupambana nae au kumuua kwani unaweza kusababisha akuume tena.

Ikiwezekana weka kumbukumbu ya muda aliokuuma na pia aina au rangi ya nyoka husika.

NB: Unapoumwa na nyoka, epuka kugusa sehemu ya jeraha na pia usioshe, kukwangua, kuchanja au kunyonya sehemu ya jeraha kwani inaweza kusababisha maambukizi au hata sumu ya nyoka kuenea kwa haraka mwilini.

Aidha, kukwangua au kuchanja sehemu ya jeraha inaweza kusababisha damu kutoka bila kukoma endapo utakuwa umeumwa na nyoka wenye sumu inayosababisha damu isigande.

Vilevile epuka kufunga kamba kuzunguka jeraha kwani inaweza kuzuia damu kupita na kusababisha kiungo husika kukatwa.
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapata matibabu kutoka katika kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe.

Credits @elimu_ya_afya

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.