Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Jinsi ya kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko

Jinsi ya kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko

Idadi ya magonjwa ya kuambukiza au magonjwa ya Mlipuko inaendelea kuongezeka; baadhi ya haya yanaibuka tena kwa kujirudia na mengine ni mapya.

Ingawa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza inayoweza kuzuilika kwa chanjo, kama vile ugonjwa wa meningococcal, homa ya manjano na kipindupindu, inaweza kuwa na athari mbaya katika maeneo yenye miundombinu duni ya afya na rasilimali, na ambapo kugundua na kutoa huduma kwa wakati ni ngumu.

Shirika la Afya Duniani(WHO) linabuni mikakati ya kimataifa ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yanayoweza kuambukizwa, kama vile homa ya manjano, kipindupindu na mafua.

Kwa kushirikiana pamoja na washirika wengine kutoka nyanja mbalimbali za kiteknolojia, kisayansi na kijamii, WHO hukusanya pamoja njia zote na mikakati inayopatikana duniani ili kukabiliana na hatari hizi za magonjwa ya Mlipuko, kisha kutoa mapendekezo yanayofaa ili kukabiliana na magonjwa haya katika ngazi za kikanda na nchi.

Jinsi ya kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko

Kwa Mujibu wa Vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa ” The Centers For diseases control and prevention-CDC’s” njia hizi huweza kutumika ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko;

✓ Kupunguza au kuondoa kabsa vitu vyote vinavyochangia tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa(antimicrobial resistance)

✓ Kupunguza au kuondoa kabsa vitu vyote vinavyochangia kuenea na kusambaa kwa magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu(zoonotic diseases) mfano Ebola

✓ Kuhamasisha Swala zima la Usafi,ikiwemo usafi wa mwili,vyakula na mazingira kwa ujumla

Moja ya njia kubwa na muhimu ya kujikinga au kuzuia kuenea kwa magonjwa ya Mlipuko kama vile kipindupindu n.k,

Ni kuhakikisha usafi wa hali ya juu, bila kusahau usafi wa mikono.

Hakikisha unanawa mikono kwa kutumia maji safi na Sabuni mara kwa mara.

✓ Kuhakikisha mazingira ya hospital ikiwemo vifaa vya hospital vinavyotumika kwa wagonjwa vinakuwa safi muda wote kabla ya kutumika.

✓ kuhakikisha Mazingira ya maabara yanakuwa Safi na yenye ulinzi wa hali ya juu, ili kuepuka kusambaa kwa vimelea vya magonjwa kutoka maabara kwenda kwa Watu.

✓ Kuhakikisha uwepo wa mpango kabambe wa Chanjo, Magonjwa mengi ya Mlipuko huweza kuzuilika kwa Kutumia chanjo.

✓ Kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ni muhimu kwa afya ya umma na usalama wa jamii. Hapa kuna hatua zingine za kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko:

1. Kufuata maelekezo ya afya kwa umma: Endelea kufuatilia maelekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya na serikali kuhusu magonjwa ya mlipuko.

Hii inaweza kuwa pamoja na ushauri kama vile wa kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kugusana na watu wengine, na kuepuka maeneo yenye msongamano wa watu.

2. Kuepuka mawasiliano ya karibu(close contact) na wagonjwa: Epuka kuwa karibu sana na watu wenye dalili za magonjwa ya mlipuko, kama vile homa, kikohozi, na mafua. Pia, kuepuka kugusa macho, pua, na mdomo kabla ya kunawa mikono.

3. Kunawa mikono mara kwa mara: Nawa mikono yako kwa maji na sabuni kwa angalau sekunde 20 kila wakati, hususan baada ya kutoka kujisaidia haja ndogo, baada ya kukohoa au kupiga chafya, na kabla ya kula.

4. Kuepuka misongamano: Epuka kukaribiana karibu na watu wengine hasa wenye dalili za magonjwa ya mlipuko,

kuepuka mikusanyiko, na kudumisha umbali wa angalau mita moja hadi mbili kati yako na mtu mwingine huweza kusaidia sana kukukinga na magonjwa ya mlipuko.

5. Kufuata maelekezo ya kusafisha na kuondoa uchafu

6. Chanjo: Endelea na ratiba ya chanjo iliyopendekezwa na wataalamu wa afya. Chanjo ni njia muhimu ya kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kulinda afya yako na ya wengine.

7. Kujitenga na wagonjwa: Watu wanaosumbuliwa na dalili za magonjwa ya mlipuko wanapaswa kujitenga na wengine ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa kwa wengine.

8. Elimu na uelewa: Jitahidi kuelimisha wengine kuhusu hatari na njia za kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko. Kutoa elimu sahihi na kutoa taarifa za kuaminika kunaweza kusaidia kuboresha ufahamu na kufanya watu wafuate miongozo ya afya.

9. Vikwanzo vya kusafiri: Katika visa vya mlipuko mkubwa, serikali inaweza kuchukua hatua za kudhibiti usafiri wa umma ili kuzuia kuenea kwa haraka magonjwa ya mlipuko, Kuzuia watu kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine hupunguza muingiliano wa watu na kuzuia kusambaa zaidi kwa magonjwa ya mlipuko.

10. Kufuatilia na kutathmini: Serikali na taasisi za afya zinapaswa kufuatilia na kutathmini hali ya magonjwa ya mlipuko ili kugundua na kudhibiti haraka maeneo yoyote ya hatari au yenye kuenea kwa kasi kwa ugonjwa.

Kumbuka, kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ni wajibu wa pamoja kwa kila mtu katika jamii. Kila mtu anapaswa kuchukua hatua za kibinafsi za kuzuia maambukizi ili kuhakikisha afya na usalama wa wote.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.