Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kisukari kwa mama mjamzito,Chanzo chake

Fahamu kuhusu kisukari kwa mama mjamzito,Chanzo chake

Kama ilivyo kwa tatizo la kisukari, pia kisukari cha mimba ni tatizo ambalo huwapata baadhi ya wanawake wakati wa kipindi cha ujauzito,

tatizo hili hupelekea kiwango cha sukari kuongezeka katika damu wakati wa ujauzito kutokana na homoni ya insulini kushindwa kufanya kazi vizuri,tatizo hili huweza kuleta athari kwa mama na mtoto endapo kiwango cha sukari hakitadhibitiwa.

Kwa kawaida wanawake wanaopata tatizo la kisukari wakati wa ujauzito hurudi katika hali ya kawaida baada ya kujifungua.

Visababishi vya kisukari cha mimba

Kwa kawaida mwili wa binadamu huzalisha homoni iitwayo insulini ambayo kazi yake kubwa ni kupunguza kiwango cha sukari katika damu hivyo kuruhusu sukari itumiwe na mwili.

Wakati wa ujauzito kuna homoni maalum kama vile projesteroni na estrojeni ambazo huzalishwa kwa wingi wakati wa ujauzito, homoni hizi hupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa homoni ya insulini hivyo kupelekea kiwango cha sukari kwenye damu kupanda hali ambayo huweza kuathiri maendeleo ya ukuaji wa mtoto na pia huweza kuathiri afya ya mama.

Vihatarishi vya kisukari cha mimba

Mwanamke yeyote anaweza kupata kisukari cha mimba, lakini wanawake ambao wako katika hatari kubwa ya kupata kisukari cha mimba ni wale ambao wana;

– Umri wa zaidi ya miaka 25 wakati wa kupata ujauzito

– Historia ya tatizo la kisukari katika familiaendapo tatizo la kisukari limekuwa likisumbua baadhi ya wanafamilia au wewe mwenyewe una tatizo la kisukari kabla ya kupata ujauzito hivyo hatari ya kupata kisukari cha mimba huwa kubwa zaidi.

– Uzito mkubwa kupita kiasi, uzito mkubwa kupita kiasi wakati wa ujauzito huongeza hatari ya kupata kisukari cha mimba.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.