Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maumivu mwisho wa kukojoa na damu kutoka

Maumivu mwisho wa kukojoa na damu kutoka

Tatizo hili la kukojoa damu huweza kutokea kwa mtu yoyote na chanzo chake huweza kuanzia popote kwenye mfumo mzima wa mkojo kama vile;

  • kwenye kibofu cha mkojo,
  • kwenye Njia ya mkojo
  • au Kwenye figo n.k.

Asilimia kubwa unaweza kupata shida ya kukojoa damu pasipo kupata maumivu yoyote, lakini ikiwa madonge ya damu yatapitishwa kwenye mkojo, hilo linaweza kukuumiza.

Chanzo cha Mtu kukojoa Damu

Hali hii ya kukojoa damu hutokea wakati figo au sehemu nyingine za njia ya mkojo zinaporuhusu seli za damu kuvuja kwenye mkojo. Sababu mbali mbali zinaweza kusababisha hali hii kutokea, Sababu hizo ni pamoja na:

– Maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo yaani UTI(urinary track infection),

Hii hutokea wakati bakteria wakiingia kwenye mrija ambao mkojo hutoka mwilini, unaoitwa urethra. Kisha bakteria huzaliana au kuongezeka zaidi kwenye kibofu.

UTI inaweza kusababisha kutokwa na damu ambapo hufanya mkojo kuonekana mwekundu au wakati mwingine rangi ya kahawia,

Ukiwa na UTI, unaweza pia kuwa na hamu kubwa ya kukojoa ambayo hudumu kwa muda mrefu. Unaweza kuwa na maumivu na kuhisi hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa. Mkojo wako unaweza kuwa na harufu kali sana.

– Maambukizi kwenye figo(Kidney infections)

Aina hii ya UTI pia inaitwa pyelonephritis. Maambukizi ya figo yanaweza kutokea wakati bakteria huingia kwenye figo kutoka kwenye damu.

Maambukizi pia yanaweza kutokea wakati bakteria huhamia kwenye figo kutoka kwenye mirija inayounganisha figo na kibofu, inayoitwa ureta,

Maambukizi ya figo yanaweza kusababisha dalili zinazohusiana na mkojo ambazo UTIs nyingine zinaweza kusababisha ikiwemo hii ya kukojoa damu. Lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha homa na maumivu.

-Jiwe kwenye kibofu au figo(bladder or kidney stone)

Madini kwenye mkojo yanaweza kutengeneza fuwele(crystals) kwenye kuta za figo au kibofu. Baada ya muda, crystals hizi zinaweza kuwa mawe magumu.

Mawe haya mara nyingi hayana maumivu, Lakini yanaweza kuleta maumivu sana ikiwa husababisha kizuizi (blockage) chochote cha mkojo kupita.

Mawe kwenye kibofu au kwenye figo yanaweza kusababisha damu kwenye mkojo ambayo inaweza kuonekana kwa macho au kuwa na kiwango kidogo sana cha damu ambayo inaweza kuonekana kwenye maabara pekee.

– Kuongezeka kwa Tezi Dume(Enlarged prostate)

Tezi hii ya prostate iko chini kidogo ya kibofu, na inazunguka sehemu ya juu ya urethra. Mara nyingi inapokuwa kubwa huweka shinikizo kwenye urethra, kisha kwa sehemu huzuia mtiririko wa mkojo.

Ukiwa na tatizo hili la kuongezeka kwa tezi dume unaweza kuwa na shida ya kukojoa,kukojoa damu n.k.

-Ugonjwa wa figo(Kidney disease)

kama nilivyosema hapo awali,unaweza kuwa na damu kwenye Mkojo ambayo unaweza kuiyona kwa macho ya kawaida,lakini wakati mwingine unaweza kuwa na kiwango kidogo sana cha damu kwenye Mkojo ambacho huwezi kukiona kwa macho ya kawaida(hapa lazima utumie vifaa maalum vya uchunguzi kama vile microscope).

Kuwepo kwa Damu kwenye mkojo ambayo inaweza kuonekana tu maabara ni dalili ya kawaida ya ugonjwa wa figo unaoitwa glomerulonephritis.

– Kuwa na tatizo la Saratani

Damu kwenye mkojo ambayo inaweza kuonekana kwa macho inaweza kuwa ishara ya saratani ya kibofu,Saratani ya figo au Saratani ya tezi dume(prostate cancer).

Saratani hizi haziwezi kusababisha dalili mapema ikiwa matibabu yameanza kufanya kazi vizuri.

– Magonjwa ya kurithi(Inherited illnesses)

Hali ya kijenetics inayoathiri chembechembe nyekundu za damu, iitwayo sickle cell anemia, inaweza kusababisha damu kwenye mkojo.

Seli za damu zinaweza kuonekana kwa macho au kuwa ndogo sana kiasi cha kutokuonekana kwa macho. Hali inayoharibu mishipa midogo ya damu kwenye figo, inayoitwa “Alport syndrome” pia inaweza kusababisha damu kwenye mkojo.

– Kuumia kwa figo(Kidney injury)

Kuumia au kupata jeraha kwenye figo kutokana na ajali au sababu zingine inaweza kusababisha damu kuonekana kwenye mkojo.

– Matumizi ya baadhi ya Dawa.

Baadhi ya dawa mfano; Dawa ya kuzuia saratani ya cyclophosphamide (Cytoxan) na antibiotics kama penicillin zinaweza kuhusishwa na tatizo hili la kuwa na damu kwenye mkojo.

Dawa zinazozuia kuganda kwa damu pia zimehusishwa na tatizo hili la damu kwenye mkojo,

Dawa Hizi ni pamoja na dawa zinazozuia chembechembe za damu zinazoitwa platelets kushikamana, kama vile aspirini ya kutuliza maumivu. Dawa zingine kama vile heparini, pia zinaweza kuwa sababu.

– Kufanya Mazoezi magumu

Kwa baadhi ya watu Kukojoa damu au kuwa na Damu kwenye mkojo inaweza kutokea baada ya kucheza michezo kama vile mpira wa miguu. Hii Inaweza kuhusishwa na uharibifu wa kibofu unaosababishwa na kupigwa.

Damu kwenye mkojo pia inaweza kutokea kwa michezo ya masafa marefu, kama vile mbio za marathoni, lakini haijulikani kwa nini. Hii pia Inaweza kuhusishwa na uharibifu wa kibofu cha mkojo au sababu zingine ambazo hazihusishi jeraha.

Endapo mazoezi magumu yamesababisha damu kwenye mkojo, hali hii inaweza kuisha yenyewe ndani ya wiki. Ukiona damu kwenye mkojo wako baada ya kufanya mazoezi haiishi, usidhani ni kutokana na kufanya mazoezi. Muone mtoa huduma wako wa afya kwa ajili ya vipimo zaidi.

– Magonjwa mengine ambayo huweza kusababisha mtu kukojoa mkojo wenye damu ni kama vile;

  • ugonjwa wa kichocho pamoja na magonjwa mengine ambayo huweza kushambulia mfumo mzima wa  haja ndogo
  • Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya zinaa n.k

Dalili za tatizo la Kukojoa Damu

DALILI ZA TATIZO HILI LA KUKOJOA DAMU NI PAMOJA NA;

– joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

– Kupata maumivu makali wakati wakukojoa

– Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

– Kukojoa damu mara kwa mara

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUKOJOA DAMU

– Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, kama chanzo ni UTI basi mtu atapata matibabu ya Uti, kama shida ni Kichocho,mgonjwa apate matibabu ya kichocho N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.