Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mgonjwa wa saratani apata uwezo wa kutabasamu tena baada ya upasuaji

Mgonjwa wa saratani amerejesha uwezo wake wa kutabasamu tena baada ya kufanyiwa upasuaji wa kiubunifu zaidi.

Daniel Kilty aliwashukuru madaktari wa upasuaji Alex Goodson pamoja na Matthew Ward kwa kumsaidia kutabasamu tena.

Daniel Kilty; Mwanamume mwenye umri wa miaka 52 kutoka Midhurst huko West Sussex,ambaye alipoteza uwezo wa  misuli kufanya kazi kama kawaida usoni mwake baada ya kugunduliwa na saratani anasema, sasa anaweza kutabasamu tena baada ya kufanyiwa upasuaji wa kiubunifu zaidi(Innovative surgery).

Daniel Kilty, alikuwa na uvimbe unaokua polepole kwenye shavu lake ambao ulizunguka na kuvamia mishipa, na kusababisha kupooza kabisa usoni ambapo kwa kitaalam tunaita “total facial paralysis”.

Hospitali ya Malkia Alexandra huko Portsmouth ilifanya upasuaji huo, ambao Bw Kilty alisema umemrudishia Kujiamini tena.

Bw Kilty,alisema:

“Sina saratani tu, lakini ninaweza kutabasamu tena.”

Daniel Kilty, kabla ya upasuaji huo Kwa mara ya kwanza aliona dalili ambazo zilionyesha kuna kitu hakikuwa sawa mnamo Desemba 2021, wakati jicho lake la kulia lilipoanza kuwasha na chakula kilikuwa kikikwama katikati ya meno yake na ndani ya shavu wakati wa kula.

“Upande wa kulia wa uso wangu ulishuka chini, nilionekana kuwa na huzuni kila wakati,” Bw Kilty alisema.

“Niliona ni vigumu sana, jinsi ambavyo watu wangenitazama – mitaani, kwenye treni, au hata nikiwa madukani – Baada ya watu kunitazama kwa muda mrefu zaidi na kusema ‘kuna kitu kibaya kuhusu jinsi unavyoonekana.’

Timu ya Wataalam 12 wa upasuaji ilifanya utaratibu wa kuondoa uvimbe huo ambao ni nadra sana kufanyika,

Dkt Matthew Ward wakati akizungumza na shirika la utangazaji la BBC alieleza jinsi upasuaji huo utakavyoboresha maisha ya Bw Kilty.

Aina hii ya upasuaji itasaidia sana kurudisha na kuunganisha nerves zinazohusika na kutafuna “chewing nerve” pamoja na nerves zinazosaidia mtu kutabasamu “smiling nerve” hali ambayo husaidia kurudisha muonekano wa kawaida wa Uso.

Bw Kilty alikuwa mgonjwa wa kwanza katika Hospitali ya Malkia Alexandra kufanyiwa upasuaji huu mahususi, unaoitwa “facial reanimation”, ambao ulianzishwa katika Chuo Kikuu cha Portsmouth Hospitals NHS Trust na madaktari wa upasuaji Alex Goodson na Matthew Ward.

Dr Matthew Ward  alieleza zaidi;

“Bila upasuaji huu, Daniel angeweza kula na kuongea vizuri, lakini anaweza kukosa ujasiri mkubwa wa kijiamini, kukosa uwezo wa kutabasamu na kuonyesha hisia akiwa peke yake au mbele za watu.”

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.