Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mtumishi Wa Afya Kituo Cha Kivule aliyekiuka maadili ya kitaaluma, asimamishwa kazi

Mtumishi Wa Afya Kituo Cha Kivule aliyekiuka maadili ya kitaaluma, asimamishwa kazi

Na. WAF, Bariadi -Simiyu.

Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amepongeza hatua iliyochukuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kwa kumsimamisha kazi mtumishi wa afya katika Kituo cha Afya Kuvule kufuatia kuonekana kwenye video akiwa akisafisha vyombo vya Hospitalini kwa njia isiyofaa.

Waziri @ummymwalimu amesema hayo leo akiwa Bariadi, Simiyu kwenye ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo amebainisha kuwa kitendo alichofanya mtumishi huyo hakikubaliki hata kidogo.

“Tumeona juzi kule Dar Es Salaam, mtumishi anaosha vyombo vya Hospitali kwa maji ya baridi na kuanika juani, sijawahi kuona na nimefurahi kuona kuna hatua imechukuliwa, hivi ni kweli mtumishi unafundishwa hivyo kuosha vyombo na kuanika juani? amesema Waziri @ummymwalimu .

Kufuatia kusambaa kwa video ya mtumishi huyo akisafisha vifaa vya Hospitalini kwa njia isiyo rasmi, mnamo Julai 8, 2023  Waziri Ummy Mwalimu alitoa tamko na kusema kuwa Mtumishi huyo alikuwa amefanya kosa kwa kukiuka Miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi wa Magonjwa (Infection Prevention and Control)

Aidha Mhe. @ummymwalimu amewasisitiza watumishi wa Afya kuzingatia weledi katika Majukumu yao ya kazi, huku akiwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wanakiuka maadili na miiko ya kazi zao.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.