Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Unywaji wa wastani wa Pombe hautapunguza hatari ya kupata kisukari au kunenepa kupita kiasi

Unywaji wa wastani wa Pombe hautapunguza hatari ya kupata kisukari(type 2 diabetes) au hatari ya kunenepa kupita kiasi(obesity)

Baadhi ya watu hudhani kwamba,matumizi ya pombe kwa Wastani hayana madhara yoyote mwilini? Je ni kweli kuna kiwango salama cha unywaji wa Pombe? Soma hapa kufahamu,

Karibu ndani ya @afyaclass lifestyle, tujifunze mtindo wa maisha salama na wenye afya.

Wataalamu wanapendekeza kwamba wanaume wasizidi vinywaji 2 vya kawaida kwa siku wakati wanawake wapunguze unywaji wa pombe hadi kinywaji 1 kwa siku.

Utafiti mpya unaonyesha kuwa hata unywaji mdogo wa Pombe hauwezi kuwa kinga dhidi ya matatizo mbali mbali kwenye endocrine kama vile kisukari aina ya 2(type 2 diabetes) na Unene au UZito kupita kiasi(Overweight/Obesity),

Kwa tafsri nyingine hata unywaji wa kiwango kidogo cha pombe bado hauwezi kuwa kinga kwa afya yako.

Unywaji wa pombe kupita kiasi unahusishwa na idadi kubwa ya matokeo mabaya ya kiafya, pombe huleta madhara mengi kwenye mwili wa binadamu, Matatizo mbali mbali ya kiafya huweza kuzidishwa zaidi kutokana na unywaji pombe.

“Wataalamu wanasema kwamba kiasi pekee cha pombe ambacho ni salama kabisa ni kuacha matumizi ya pombe”.(the only truly safe amount of alcohol is no alcohol).

Utafiti huo ulichapishwa katika Jarida la Endocrine Society of Clinical Endocrinology & Metabolism, ambapo;

Watafiti walisema matokeo yao yalionyesha madhara ya unywaji wa pombe – hata unywaji wa kiwango kidogo hadi wastani – linapokuja suala la afya ya endocrine.

Wataalamu waliohojiwa na jarida la “Medical News Today” wanasema utafiti huo unatumika kama ukumbusho kwamba; kiwango pekee na salama cha pombe sio kutumia pombe hata kidogo.

Madhara ya kiafya ya pombe

Inafahamika kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni mbaya na ndio chanzo kikuu cha vifo vinavyoweza kuzuilika.

Hata hivyo, hekima ya kawaida inasema kwamba kunywa kidogo – kama vile glasi ya divai kwa siku – kuna faida za afya.

Dk. Tianyuan Lu, mwandishi mkuu wa utafiti huo na mtaalamu wa magonjwa katika Chuo Kikuu cha McGill huko Montreal, Quebec, Kanada, aliiambia Medical News Today kwamba takwimu hizo zinatoa ushahidi wa kutosha kwamba unywaji wa pombe hata kiwango kidogo hauwezi kupunguza hatari ya kupata kisukari aina ya pili (type 2 diabetes) au hatari ya kunenepa kupita kiasi(obesity).

Anasema;

“Heavy drinking has been associated with multiple adverse health outcomes, which is what we confirmed in this study,” Dk. Tianyuan Lu said. “However, there has been a long-standing debate on whether light drinking has protective effects. Our study found that light drinking does not protect against obesity or type 2 diabetes.”

Watafiti walikusanya data au takwimu kutoka kwa zaidi ya washiriki 400,000 wa utafiti kutoka U.K. Biobank.

Watafiti waliripoti kuwa watu wanaokunywa zaidi ya vinywaji 14 kwa wiki walikuwa na hatari kubwa ya kupata tatizo la unene kupita kiasi(obesity) na ugonjwa wa kisukari aina ya pili(type 2 diabetes).

Hata hivo, Miongoni mwa wale ambao walikunywa vinywaji 7 au chini ya hapo kwa wiki, hakukuwa na ushahidi wowote wa kuwa na matokeo bora ya afya.

Dk. Tianyuan Lu alitahadharisha kuwa ingawa utafiti unahitimisha kuwa unywaji wa pombe kwa kiwango kidogo hauna matokeo yoyote ya kinga, hii haipaswi kuchanganywa na unywaji mdogo wa Pombe kuwa na athari mbaya kiafya.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.