Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Vitu vya kuepuka ukiwa mjamzito,Fahamu hapa

Vitu vya kuepuka ukiwa mjamzito,Fahamu hapa

Kila mzazi anataka kumpa mtoto wake mwanzo bora zaidi maishani, na ni jambo unaloweza kufanyia kazi kabla mtoto wako hajazaliwa. Mwili wako unapobadilika, baadhi ya tabia zako zinaweza kuhitaji kubadilika pia.

Hapa kuna vidokezo kuhusu mambo ya kuepuka wakati wa ujauzito ili kusaidia kumuweka mtoto wako aliyetumboni salama zaidi.

Vitu vya kuepuka ukiwa mjamzito,Fahamu hapa

1. Epuka matumizi ya dawa hovyio Pasipo maelekezo kutoka kwa Wataalam wa afya

2. Epuka kuvaa nguo za kukubana sana, Mikanda tumboni, au Viatu virefu sana(high heels)

3. Kuhusu Matumizi ya Vyakula;Vyakula vya kuepuka wakati wa ujauzito,

Hakikisha unapata Mlo kamili(Mlo wenye Virutubisho vyote muhimu kwenye kiwango sahihi kinachohitajika mwilini) na Mlo salama, hii ni muhimu sana kwa Usalama na maendeleo bora ya Ujauzito wako. Ili kuzuia maambukizi hatari, tunapendekeza yafuatayo:

  • Usitumie Maziwa ambayo hayajachemshwa
  • Usitumie vyakula vilivyokwisha muda wake wa matumizi(expired foods)
  • Usile nyama ambayo haijapikwa, hakikisha nyama inapikwa vizuri
  • Usile samaki au vyakula vya baharini ambayo havijapikwa
  • Usile mayai mabichi

– Epuka kula kitu chochote bila kunawa Mikono, Hakikisha unanawa Mikono kwa maji safi na Sabuni kabla ya Kula

– Hakikisha vyombo vyote vya kula chakula ni Safi

4. Epuka Matumizi ya Pombe wakati wa Ujauzito

Huenda umesikia kuwa unywaji wa pombe wakati wa ujauzito ni hatari, na hii ndiyo sababu: Watoto walioathiriwa sana na pombe wakiwa tumboni wana hatari kubwa ya kuathiriwa kwenye ukuaji wao na wanaweza kupata matatizo ya neva,kuzaliwa na tatizo la uzito Mdogo n.k.

5. Epuka Uvutaji wa Sigara ukiwa Mjamzito

Inaweza kuwa vigumu kuacha kuvuta sigara, lakini kumlinda mtoto wako dhidi ya moshi wa tumbaku ni muhimu sana ili kumpa mtoto wako mwanzo mzuri maishani. Kuvuta sigara kunaweza kuzuia usambazaji wa oksijeni kwa mtoto wako na huongeza hatari ya Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.

Watoto ambao wazazi wao huvuta sigara pia wana uwezekano mkubwa wa kupata tatizo la pumu na magonjwa mengine makubwa. Ili kupata usaidizi wa kuacha tumbaku, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya. TIPS kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) zinapatikana pia mtandaoni.

6. Epuka matumizi ya Vitu vyenye Caffeine nyingi wakati wa Ujauzito

Ingawa inaweza kuwa vigumu kuacha matumizi ya chai au kahawa, inashauriwa kufuatilia ulaji wako wa kafeini kwa miezi tisa ya Ujauzito. Chai,kahawa au Vinywaji vingine huweza kuwa ni kiwango kikubwa cha caffeine,

Kiasi kikubwa cha kafeini huzuia ukuaji wa Mtoto tumboni, na inashauriwa kuwa wanawake wajawazito wasizidi 200 mg kwa siku. Kiasi cha kafeini katika vyakula na vinywaji hutofautiana, kwa hivyo hakikisha kusoma lebo za vyakula unavyokula ili kujua kiwango cha caffeine kilichopo ndani.

7. Hata kama huvuti Sigara, Epuka kabsa kuwa haribu na watu wanaovuta sigara, ili kujikinga na moshi wa Sigara kutoka kwa watu wengine(second-hand smoke)

8. Epuka kunyanyua Vitu vizito Sana wakati wa Ujauzito N.k

NB: Ni muhimu sana Kwa Mama mjamzito kuhudhuria kliniki Zote ili kuhakikisha yeye pamoja na Mtoto aliyetumboni wanakuwa Salama;

Kuna Mahudhurio Manne ya Kliniki kwa mama Mjamzito(four visits),endapo mama huyu hana changamoto yoyote kwenye Ujauzito wake;

  1. Hudhurio la kwanza,Ujauzito kabla haujafikia wiki 16
  2. Hudhurio la Pili, wiki 20 mpaka 24
  3. Hudhurio la Tatu, wiki 28 mpaka 32
  4. Hudhurio la Nne, wiki 36 mpaka 40

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.