Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Bodybuilder amuua mke wa zamani live INSTAGRAM Kwa kumpiga risasi kichwani mbele ya binti yao

Mwanaume mmoja anayejishughulisha na mazoezi ya kujenga mwili(Bodybuilder) wa Bosnia alifanya mauaji ya mke wake wa zamani moja kwa moja akijionyesha LIVE INSTAGRAM wakati wa kutokea shambulizi la risasi na kuwaua wengine wawili na kisha yeye mwenyewe.

Mwanamume huyo, aliyetambuliwa kama Nermin Sulejmanovic alionyesha video ya kutatanisha kwa mara ya kwanza kwenye Instagram mnamo Ijumaa asubuhi, Agosti 11, akiwaambia watazamaji kwamba wangeona mauaji moja kwa moja.

Kisha video hiyo inamuonyesha akichukua bunduki na kufyatua risasi kwenye paji la uso la mwanamke. Mtoto wa kike wa wanandoa hao pia anasikika akilia kwenye video hiyo.

Sulejmanovic, 35, alithibitisha kuwa amemwacha mtoto mchanga akiwa hai.

Mtuhumiwa wa mauaji baadaye alisema: ‘Nilimwonya kila mtu kwamba ingefikia hivi. Amekuwa akimficha mtoto wangu kwa siku nane.

‘Nasubiri kupakia silaha yangu na kuendelea.’

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, Sulejmanovic alifanya kazi kama mkufunzi wa mazoezi ya viungo lakini pia alikuwa mwanachama wa genge na alikuwa na hatia kadhaa kwa vitendo vya vurugu, mapigano, na kuhusika kwake katika ulanguzi wa dawa za kulevya.

Wakati polisi wakianza kumsaka kufuatia mauaji hayo yaliyotangazwa, mshukiwa baadaye alichapisha video nyingine kwenye mtandao wa Instagram, akidai kuwapiga risasi watu wengine wawili wakati akitoroka.

Taarifa ya polisi katika mji wa Tuzla kaskazini mashariki mwa Bosnia ilisema kuwa mbali na watu watatu waliouawa, watu wengine watatu walijeruhiwa kabla ya muuaji huyo ‘kujiua baada ya kupatikana na kabla ya kukamatwa’.

Polisi hawakutoa maelezo zaidi mara moja, lakini wakaongeza kuwa watu ambao waliandika ujumbe wa kumuunga mkono wakati wakibofya machapisho ya mtu huyo kwenye Instagram Ijumaa watahojiwa na huenda wakakabiliwa na hatua za kisheria.

“Sina maneno ya kuelezea kile kilichotokea leo huko Gradacac,” alisema Nermin Niksic, Waziri Mkuu wa Shirikisho la Bosnia.

‘Muuaji alijiua mwishowe, lakini hakuna anayeweza kurejesha maisha ya wahasiriwa.’

Mamlaka haikutoa mara moja maelezo zaidi au sababu zinazowezekana za ufyatuaji risasi.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.