Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Nyonga na Goti kutoka Marekani Dkt. Steve Mayer na Dr.mollel
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Nyonga na Goti kutoka Marekani Dkt. Steve Mayer na Dr.mollel:
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel @dr_mollel jioni ya jana amekutana na kufanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Nyonga na Goti kutoka Marekani Dkt. Steve Mayer ambaye amekuja kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa nchini.
Dkt. Mayers amembana na madakari wengine 55 kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma za kubadilisha nyonga na goti.
Serikali ya Rais Dkt Samia inaendelea kufungua mipaka yake nje zaidi kuleta karibu huduma za kibingwa ambapo watalaam hawa watatoa huduma hizo za matibabu bure katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kuanzia kesho tarehe 11 hadi 17 Agosti, 2023.
Katika mazungumzo hayo Dkt. Mollel ameongozana na mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambaye ameratibu ujio wa madaktari hao.