Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Dkt. Samia Suluhu leo hii Agosti 13, 2023 amewakaribisha Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka nchini Marekani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo hii Agosti 13, 2023 amewakaribisha Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka nchini Marekani katika hafla ya chakula cha mchana Ikulu Chamwino Dodoma.

Rais @SuluhuSamia amewashukuru madaktari hao kwa moyo wao wa kujitolea kuwasaidia Watanzania kupata huduma za matibabu ya kibingwa.

Madaktari hao bingwa wameweka kambi katika Hospitali ya Serian Lutherani Jijini Arusha ambapo wanatoa matibabu ya kubadilisha nyonga na goti bure kuanzia Agosti 11 mpaka 17, 2023.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia Waziri wa Afya Mhe. @UmmyMwalimu, Viongozi waandamizi wa Wizara Taasisi za Afya, Madaktari pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Afya nchini.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.