Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Fahamu Aina, Faida pamoja na Hasara za Akili bandia (Artificial Intelligence)

Akili bandia (AI) ni programu ya kompyuta yenye uwezo wa kijifunza na kufanya kazi zinazohitaji utashi wa binadamu.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, mchambuzi wa masuala ya akili bandia Zephania Reuben amesema kuna aina tatu za akili bandia ambazo ni Artificial Narrow Intelligence ambayo hufanya kazi maalumu kama kutambua picha ya mtu fulani na kuweza kutofautisha kati ya picha X na picha Y.

Aina nyingine ni Artificial General Intelligence ambayo hufanya kazi kwa utashi kama binadamu na ya mwisho ni Artificial Super Intelligence inayofanya kazi kuliko uwezo wa bindamu na kwa ubora zaidi.

Aidha, mchambuzi huyo wa masuala ya akili bandia ametaja faida za matumizi ya akili bandia katika sekta mbalimbali.

Ametolea mfano katika sekta ya kilimo ambapo akili bandia inaweza kuwasaidia Wakulima kujua magonjwa yanayosumbua mazao na pia katika utabiri wa hali ya hewa.

Zephania amesema katika sekta ya afya
Artificial Intelligence inasaidia kugundua magonjwa, huku katika uchumi ikitajwa kuwa na uwezo wa kugundua miamala isiyo salama .

Kwa upande wa hasara amesema matumizi ya akili bandia mfano katika habari yanaweza kutoa habari zisizo sahihi na kwa upande wa elimu inapunguza ubunifu kwa Wanafunzi kwa kuwa inawafanya kutegemea zaidi akili bandia.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.