Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

GOLIKIPA wa Simba SC, Ally Salim Khatoro ameibuka shujaa (The hero) baada ya kudaka penalti tatu

GOLIKIPA wa Simba SC, Ally Salim Khatoro ameibuka shujaa (The hero) baada ya kudaka penalti tatu kwenye mchezo wa Fainali ya mashindano ya Ngao ya Jamii 2023 dhidi ya Yanga SC kwenye dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Katika mchezo huo, Simba SC wameibuka kidedea kwa jumla ya mikwaju ya penalti 3-1 dhidi ya mtani
wao Yanga SC baada ya sare ya 0-0 kwenye dakika 90′ za mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki wa soka kwenye dimba hilo la Mkwakwani.

Changamoto ya mikwaju ya penalti ilifuata baada ya sare hiyo tasa kwenye dakika hizo 90. Simba SC walianza kupiga mkwaju wao wa penalti kupitia kwa Kiungo wao, Mzamiru Yassin Selemba ambaye alimpoteza maboya Golikipa wa Yanga SC, DiiguiDiarra.

Yanga SC walipiga mkwaju wao wa kwanza kupitia kwa Stephane Aziz Ki ambaye alipiga vizuri mkwaju huo na kuweka wavuni akimuacha Golikipa Ally Salim hana la kufanya. Simba SC walipiga mkwaju wao wa pili kupitia kwa Saido Ntibazonkiza ambaye alikosa kwa Diarra kupangua vizuri.

Kiungo Khalid Aucho alikosa mkwaju wa penalti wa pili baada ya Ally Salim (The hero) kudaka na kuuficha kabisa mpira wa Aucho uliopigwa upande wake wa kulia.

Simba SC nao walikosa mkwaju wa tatu baada ya Moses Phiri kuupeleka juu ya lango mpira.

Mkwaju wa tatu wa penalti wa Yanga SC uliopigwa na Kiungo Pacôme Zouzoua ambaye alikosa kwa mkwaju wake kupanguliwa na Ally Salim. Penalti ya nne ya Simba SC ilipigwa na Mshambuliaji Onana Essomba Willy ambaye alipata kwa kumuacha Kipa Diarra hana la kufanya.

Mlinzi wa kulia wa Yanga SC, Kouassi Attohoula Yao alikosa mkwaju wa nne ambao ulipanguliwa tena na Ally Salim. Mkwaju wa ushindi kwa upande wa Simba SC ulipigwa na Mshambuliaji Jean Baleke ambaye alimuacha Diarra hana la kufanya kudaka mkwaju huo.

Mchezo wa awali vwa kusaka nafasi ya tatu wa Ngao ya Jami uliisha kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars
kwenye huo huo wa CCM Mkwakwani.
Katika mchezo huo mabao ya Azam yalifungwa na Washambuliaji Prince Dube kwenye dakika ya 1′ na Abdul Suleiman Sopu dakika ya 42:

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.