Hizi hapa ni Dalili muhimu sana kujua za presha ya macho maarufu kama Glaucoma
Fahamu Moja ya Vitu vya muhimu sana kwa mtu mwenye Presha ya macho ni kuhakikisha anaanza Tiba mapema, Hivo ni muhimu sana kutambua dalili mapema ili endapo zimejitokeza uwahi mara moja kwenye vipimo.
Hizi hapa ni Dalili muhimu sana kujua za presha ya macho maarufu kama Glaucoma;
1. Kuona rangi ya upinde wa mvua wakati unapoangalia taa
2. Kupungua uwezo wa kuona kwa pembeni
3. Kupoteza uwezo wa kuona kabsa
4. Macho na kichwa kuuma
5. Macho kuwa makubwa ua kioo cha jicho kuwa cheupe (Kwa watoto)
Nb; Pima macho angalau mara moja kwa mwaka ili kubaini kama una matatizo yoyote ya macho mapema
” Dunia ni angavu, tunza uoni wako”
Afya yangu,Mtaji wangu
Soma zaidi hapa: Kuhusu Ugonjwa wa Presha ya Macho