Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jinsi Stress zinavyosababisha tatizo la Presha na vitu vya kufanya ukiwa kwenye hali hii

Jinsi Stress zinavyosababisha tatizo la Presha na vitu vya kufanya ukiwa kwenye hali hii

Kuna uhusiano wa karibu kati ya kuwa na Stress pamoja na tatizo la shinikizo la juu la damu(high blood pressure)

Stress zinaweza kupandisha presha, na pia zina uhusiano wa karibu na kuleta madhara makubwa kwenye afya ya moyo pamoja na mishipa ya damu “cardiovascular health”.

Kujifunza jinsi ya kudhibiti Stress kunaweza kuleta mabadiliko katika afya kwa ujumla, na kunaweza kupunguza shinikizo la juu la damu (hypertension),

Soma ili upate maelezo zaidi kuhusu uhusiano kati ya stress za muda mrefu kwenye shinikizo la damu na baadhi ya vidokezo vya kudhibiti tatizo la Stress.

Jinsi Stress zinavyoweza kusababisha Presha

Stress zinaweza kuwa za muda mfupi (acute) au muda mrefu(chronic). Stress za muda mfupi huweza kutokana na baadhi ya vitu kama vile;

  • Wakati umeenda kwenye mazingira ya hospital,unajikuta unaogopa au kuwa na stress, hali ambayo huondoka mara tu baada ya kutoka kwenye mazingira yale
  • Kuwa na hali ya Stress kabla ya kutoa speech kwa watu au kufanya maumuzi juu ya jambo flani n.k

Stress za muda mrefu huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

  • Mahusiano ya kimapenzi
  • Matatizo ya kifedha
  • Kutokuwa na chakula ndani/njaa
  • Stress zinazotokana na kazi unayofanya n.k

Sasa kwa Ujumla, bila kujali Stress ni za muda mfupi au muda mrefu, hali ya Stress huathiri mfumo wa utendaji kazi wa Moyo pamoja na mishipa ya damu(cardiovascular system) kwa kubadilisha viwango vya vichocheo(hormone levels) mwilini.

Hormones zinazozalishwa mwilini ukiwa kwenye hali ya stress huweza kuathiri afya ya mwili mzima ikiwemo na Presha ya damu(The body’s fight-or-flight response),

Wakati upo kwenye Stress mwili hujiandaa kukabiliana na hali iliyopo kwa njia mbili; kupambana na hali iliyopo kwa kuikabili moja kwa moja au kukimbia kutoka kwenye hatari.

Wakati mtu anapokutana na hatari au vitu vinavyomsababishia Stress, Mfumo wa fahamu ambao ni “sympathetic nervous system” huhamasisha tezi aina ya adrenal glands kuzalisha vichecheo(Stress hormones) ambavyo ni adrenaline and cortisol.

Vichocheo hivi huuweka mwili tayari kukabiliana na hali iliyopo, na matokeo yake husababisha mabadiliko haya mwilini;

1. Kuongeza Mapigo ya Moyo

2. kuongeza kiwango cha Upumuaji(breathing rate), kuvuta hewa ndani na kutoa nje

3. Kutanua Zaidi njia ya hewa

4. Kuongeza presha ya Damu

5. Kuongeza mtiririko wa damu kwenye misuli ya mwili, na kupunguza mtiririko wa damu kwenye viungo vinavyohusika na umeng’enyaji chakula(digestive organs).

KUMBUKA: kuongezeka Presha kwa muda mfupi ukiwa kwenye hali ya Stress za muda mfupi ni hali ya kawaida na hutarajiwa kutokea hivo,

Ndyo maana kwa hali yoyote ile unashauriwa kupima Presha yako baada ya kukaa kutulia angalau kwa dakika 5 kabla ya vipimo ili kupata majibu sahihi, Upimaji wa Presha unatakiwa kufanyika mwili ukiwa kwenye hali ya kutulia zaidi(hali ya kawaida ya mwili).

Ukiwa hata na Stress kidogo tu au hali ya wasi wasi hata kwa kumuona tu daktari au kuwa tu kwenye mazingira ya hospital inaweza kusababisha ongezeko la presha yako, Hata kutembea tu kutoka sehemu ulipo kaa mpaka kwenye chumba cha vipimo huweza kusababisha presha ikaongezeka.

Kwa Upande wa Stress za Muda mrefu madhara yake huweza kuwa makubwa Zaidi,

Mpaka sasa ni ngumu kudhibitisha Uhusiano wa moja kwa moja kati ya Stress za muda mrefu/sugu na shinikizo la damu la muda mrefu. Hata hivyo, tafiti zimeonyesha kuwa,Stress za muda mrefu/kudumu hazihusiani tu na kuongeza presha(shinikizo la juu la damu), bali pia na aina nyinginezo za magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kama vile mashambulizi ya moyo(heart attacks) pamoja na kiharusi(Stroke).

NB: Stress haziepukiki, lakini jinsi unavyokabiliana na Stress ni jambo muhimu zaidi katika kuleta matokeo kwenye afya yako.

• JINSI YA KUPUNGUZA STRESS, Soma Zaidi hapa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.