Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Karibu watoto 500 wamefariki kutokana na njaa Sudan kwa mujibu wa Shirika la Save the Children

Karibu watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan kwa mujibu wa Shirika la Save the Children.

Shirika la kimataifa la hisani la Save the Children limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan.

Shirika la kimataifa la hisani la Save the Children limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan, wakiwemo watoto zaidi ya 20 katika kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali katika mji mkuu Khartoum, tangu mapigano yalipozuka nchini humo mwezi Aprili.

Shirika la Save the Children pia lilisema kuwa karibu watoto 31,000 wanakosa huduma ya lishe na matibabu ya utapia mlo tangu shirika hilo la misaada kusitisha shughuli zake kwenye vituo 57 vya lishe nchini Sudan.

Mzozo huo wa Sudan umegeuza jiji la Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa viwanja vya vita. Wakazi wengi wanaishi bila maji na umeme, na mfumo wa huduma za afya nchini humo umekaribia kuporomoka.

Arif Noor, mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Sudan amesema hawakutegemea kuwaona watoto wakifa kwa njaa katika idadi na hali kama hiyo. Noor amesema wameshuhudia watoto wakifa njaa inayoweza kuzuilika kabisa. Amesema idadi ya watoto walioachishwa shule nchini Sudan pia imeongeza.

Credit:dw_Swahili

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.