Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Maadhimisho ya Siku ya Watoto Wanaozaliwa Utumbo ukiwa nje ( Gastrochisis)

Jamii yatakiwa kuzingatia miongozo ya afya katika kipindi cha ujauzito ili kukabiliana na tatizo la watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje na kuhakikisha wanapatiwa matibabu kwa wakati.

Wito huu umetolewa na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga wakati wa Maadhimisho ya siku ya Watoto Wanaozaliwa utumbo ukiwa nje, Dkt. Massaga ameiomba jamii kuendelea kuhamasisha uelewa wa tatizo la watoto wanaozaliwa Utumbo nje ili kuwahakikishia usalama wa watoto hao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Dkt. Massaga amewasisitiza Wakina mama chini ya miaka 25 ambao ndio kundi linalotajwa kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili la kujifungua watoto wenye utumbo ukiwa nje kufanya kipimo cha Ultra Sound ili kujua kama wana tatizo au hawana na wakikutwa na tatizo wahakikishe wanajifungua katika Hospitali zenye uwezo wa kuhudumia watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje na kwa Kanda ya Ziwa huduma hii inatolewa katikati Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando pekee.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za upasuaji na Daktari Bingwa wa upasuaji wa watoto Dkt. Sr. Alicia Masenga ameihasa jamii kutowanyanyasa watoto wanaozaliwa na tatizo hili wala kuwakatia tamaa kwani tatizo hili likishughulikiwa kwa wakati linatibika.

Wakitoa shuhuda zao wahanga wa tatizo hili wameishukuru Hospitali ya Bugando kwa juhudi kubwa wanazofanya kuokoa maisha ya watoto wao na kuwaomba waendelee kusaidia na wengine kama watoto wao walivyotibiwa.

 

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.