Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mbegu za kiume pamoja na Yai huishi muda gani?

Mbegu za kiume pamoja na Yai huishi muda gani?

Mbegu za kiume haziwezi kuishi kwa muda mrefu ziwapo kwenye mazingira ya nje ya mwili,

Kwa hakika ni muda gani mbegu za kiume zinaweza kuishi inategemea mazingira ambayo zipo na jinsi umajimaji unaozunguka seli za manii hukauka haraka.

Mbegu za kiume huishi muda gani?

Muda wa mbegu za kiume kuishi ziwapo ndani ya mwili wa Mwanamke,

Baada ya kumwaga, mbegu za kiume au manii zinaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa takriban siku 5. Majimaji katika njia ya uzazi ya mwanamke yana virutubisho vyote ambavyo mbegu za kiume/manii huhitaji kwa ajili ya kuishi wakati huo.

Mara tu zikiwa ndani ya njia ya uzazi ya mwanamke, Mbegu za kiume au manii lazima ziogelee kupitia mlango wa uzazi(cervix) na kuingia kwenye uterasi ili kufika kwenye mirija ya uzazi na yai la Mwanamke. Ni safari ndefu sana kwa seli za manii kufanya hivo na ni chache sana zinazoendelea kuishi.

Afya ya Mbegu za Kiume au manii

Zipo Sababu nyingi zinazoweza kuathiri mchakato mzima wa utengenezaji wa mbegu za kiume/manii. Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume au utendakazi duni wa manii ni pamoja na:

(1) Afya na Mtindo wa Maisha kwa Ujumla,ikiwa ni pamoja na;

  • Matumizi ya Dawa ikiwemo dawa za kulevyia
  • Unywaji wa Pombe
  • Aina ya kazi unayofanya
  • Uvutaji wa Sigara
  • Matumizi ya Tumbaku
  • Kuwa na Msongo wa mawazo
  • Korodani kupata joto kupita kiasi
  • Kuwa na Uzito mkubwa/kupita kiasi

(2) Sababu za kimazingira,ikiwemo;

  • Kuwa kwenye mazingira ya kemikali za viwandani(industrial chemicals)
  • heavy metals
  • Mionzi(radiation au X-rays)

(3) Sababu za Kiafya(Medical reasons)

  • Maambukizi ya magonjwa kwenye Korodani
  • Saratani ya korodani
  • Kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya Veins, ambayo hutoa damu kutoka kwenye korodani
  • Tatizo la hormone imbalances
  • Shida kwenye mirija ambayo hubeba manii(mbegu za kiume) kwenye mfumo wa uzazi
  • Sababu za kigenetic(chromosomal or genetic disorders)
  • Matumizi ya baadhi ya dawa
  • Kufanyiwa Upasuaji ambao huhusisha nyonga,tumbo au viungo vya Uzazi n.k

Yai huishi muda gani?

Kitendo cha yai kutoka kwenye vifuko vyake(Ovulation) huchukua takriban siku 1 pekee,

Vichocheo vya mwili husababisha yai litoke kwenye vifuko vyake(Ovaries) kisha kuingia kwenye mirija ya Uzazi,kwa kitaalam fallopian tubes.

Wakati Yai limeanza Safari yake kuelekea kwenye kizazi au mji wa mimba huweza kuwa HAI kwa muda wa Siku Moja pekee,

Baada ya Yai kutoka kwenye vifuko vyake(kitendo ambacho hujulikana kama Ovulation) huweza kuishi kwa muda wa saa 12 mpaka 24 tu, na kwa wakati huu lazima mayai haya yarutubishwe kama mwanamke anahitaji kubeba Ujauzito.

Hitimisho

Kwa kumalizia,Baada ya kumwaga, mbegu za kiume au manii zinaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa takriban siku 5, Na baada ya Yai kutoka kwenye vifuko vyake(kitendo ambacho hujulikana kama Ovulation) huweza kuishi kwa muda wa saa 12 mpaka 24 pekee.

Huo ndyo Muda ambao mbegu za Mwanaume na mayai ya mwanamke huweza kuishi endapo yapo ndani ya Mwili.

Source:

1. MedicalNewsToday

2. The Womens

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.