Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mzunguko wa hedhi ni nini? Fahamu zaidi juu ya mzunguko wako wa hedhi

Mzunguko wa hedhi ni wakati kutoka siku ya kwanza ya hedhi ya mwanamke hadi siku kabla ya hedhi inayofuata.

Kipindi cha hedhi ni kipindi ambacho damu ya kila mwezi hutoka kwenye uke ambayo hutokea mwanzoni mwa kila mzunguko wa hedhi. Wakati wa hedhi, safu ya uterasi hutoka na kutolewa kama damu ya hedhi.

Katika mzunguko wa hedhi:

Yai hukomaa na kutolewa, mchakato huu kitaalamu huitwa (ovulation).

Utando wa mfuko wa uzazi huvimba na mishipa ya damu, hivyo huwa tayari kupokea yai lililorutubishwa na mbegu ya kiume.

Yai lililorutubishwa hushikamana na utando wa uterasi na kuanza kukua.

Lakini, endapo yai halijarutubishwa hushindwa kushikika kwenye utando wa uterasi, hivyo hutolewa kama damu ya hedhi.

Urefu wa mzunguko wa hedhi hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, lakini wastani ni kuwa na hedhi kila baada ya siku 28. Mzunguko wa hedhi kawaida huchukua kati ya siku 23 na 35 lakini unaweza kutofautiana kutoka mwezi hadi mwezi. Kawaida, hedhi huchukua siku 3 hadi 7.

Wasichana huanza kupata mzunguko wa hedhi wakati wa kuvunja ungo, wakiwa na umri kuanzia miaka 13, na kipindi hicho cha hedhi hukoma wakiwa na umri wa miaka 52.

Ovari hutoa yai (ovulation) takriban siku 14 kabla ya mwanzo wa hedhi kwa mzunguko wa siku 28.

Mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kupata mimba ikiwa atafanya ngono bila kinga wakati wa siku 3 kabla ya ovulation (kama siku 17 kabla ya kuanza kwa hedhi)

matatizo unayoweza kupata kwenye mzunguko wa hedhi

matatizo ya mara kwa mara kwenye mzunguko wa hedhi ni pamoja na:

  • Kutokwa na damu nyingi au kutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku 7
  • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.
  •  Ugonjwa kabla ya hedhi PMS (premenstrual syndrome)
  • Kukoma kwa hedhi mapema

Sababu za kawaida zinazopelekea hedhi kuacha kutoka ni kama vile:

  • Mimba
  • Kukoma hedhi

    NB: Tofauti na sababu hizo hedhi ikiacha kutoka hilo ni tatizo unapaswa kumuona mtaalamu wa afya kwa matibabu.

KWA USHAURI ZAIDI ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.