Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ombi linalotaka kupigwa marufuku kwa TikTok nchini Kenya limewasilishwa bungeni

Ombi linalotaka kupigwa marufuku kwa TikTok nchini Kenya limewasilishwa bungeni likitaja uvunjaji wa kanuni ya faragha na maudhui ya ngono, tovuti ya binafsi ya Star imeripoti.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula alisema ombi hilo lililowasilishwa na Bob Ndolo, lilidai kuwa TikTok ilikuwa ikikusanya data muhimu kutoka kwa watumiaji wake, ikiwa ni pamoja na eneo na historia ya kuperuzi

Mlalamikaji pia amesema jukwaa hilo “linakuza vurugu, lugha chafu, maudhui ya ngono na matamshi ya chuki”.

Agosti 2, serikali ilisema kwamba itapitia sheria za mtandao ili kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja katika TikTok wakati wa usiku ambapo watumiaji wanadaiwa kupeperusha maudhui ya lugha chafu.

Kenya inaongoza ulimwenguni kwa matumizi ya TikTok.

Source;BBC

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.