Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Papa Francis asikitishwa na idadi ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean,ni ”jeraha la wazi”

Mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis amesema Jumapili kwamba idadi ya wahamiaji wanaofia kwenye bahari ya Mediterranean ni ”jeraha la wazi”, kwa ubinadamu baada ya wiki nzima iliyogubikwa na mfululizo wa ajali za boti.

Katika ibada ya kila wiki ya Angelus, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 aliwaombea watu 41 walioripotiwa kupotea Jumatano na wenzao wanne walionusurika na kupelekwa kwenye kisiwa cha Italy cha Lamepdusa.

Papa alisema ni “maumivu na aibu” akikumbuka takwimu za Umoja wa Mataifa, zikionyesha kwamba zaidi ya wahamiaji 2,000 wamekufa kwenye bahari ya Mediterranean tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Wakati huo huo pia aliwapongeza wote wanaojihusisha na kuzuia ajali za boti pamoja na uokozi.

Msemaji wa shirika la UN linaloshughulikia wakimbizi, IOM mwishoni mwa wiki alisema kwamba takriban watu 2,060 wamekufa kwenye bahari ya Meditarrenean tangu mwanzo wa mwaka, wakati 1,800 miongoni mwao wakipoteza maisha katikati ya bahari hiyo kati ya Afrika kaskazini kuelekea Italy na malta.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.