Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Putin avunja ukimya kuhusu kifo cha Prigozhin

Putin avunja ukimya kuhusu kifo cha Prigozhin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amevunja ukimya wake kuhusu ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin na maafisa wengine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amevunja ukimya wake kuhusu ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin na maafisa wengine.

Katika maoni yake yaliyorushwa na televisheni za Urusi, Putin ametoa rambirambi zake za dhati kwa familia za wahanga wote, na kuelezea ajali hiyo kama janga.

Aidha, Rais Putin amemtaja Prigozhin kama mtu aliyekuwa na talanta, mtu mwenye hatima ngumu na aliyefanya makosa makubwa katika maisha yake lakini pia akimsifu kuwa mtu aliyetoa matokeo yanayohitajika. Ameongeza kuwa uchunguzi wa ajali hiyo utachukua muda, lakini utafanywa kwa ukamilifu na kufikia tamati.

Shirika la usafiri wa anga la Urusi lilisema kuwa Prigozhin pamoja na kamanda wa juu wa kundi la Wagner Dmitri Utkin, walikuwa miongoni mwa abiria 10 waliofariki kwenye ajali ya ndege iliyoanguka Jumatano.

Source:dw_swahili

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.