Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Shule yafungwa India baada ya mwalimu kuamuru wanafunzi wamchape vibao mwanafunzi wa Kiislamut

Shule yafungwa India baada ya mwalimu kuamuru wanafunzi wamchape vibao mwanafunzi wa Kiislamut

Mamlaka katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India imefunga shule ya binafsi baada ya mwalimu kuwataka wanafunzi kumpiga makofi mwanafunzi mwenzao Muislamu.

Maafisa walisema Shule ya Umma ya Neha ilifungwa kwa vile “haikukidhi vigezo vya idara ya elimu.”

Wanafunzi wa shule hiyo watahamishwa hadi shule ya serikali au shule nyingine zilizo karibu, maafisa walisema.

Wakati huo huo, mwalimu Tripta Tyagi amekiambia kituo cha habari cha NDTV kwamba “hajutii” vitendo vyake.

Familia ya mtoto huyo imesema alipigwa kwa kosa la kukosea. Video ya Bi Tyagi akiwaambia wanafunzi wake wampige kofi mwenzao Mwislamu mwenye umri wa miaka saba katika shule ndogo ya binafsi katika wilaya ya Muzaffarnagar ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii wikendi. “Mbona mnampiga kidogo hivi? Mpigeni zaidi,” anasikika mwalimu akiwaambia watoto, huku mvulana akiwa amesimama akilia.

“Mgonge mgongoni… Uso wake unageuka kuwa mwekundu, kwa hivyo mpige mgongoni sasa,” aliongeza.

Baba wa mwathiriwa aliripoti kisa hicho kwa polisi na kumtoa nje ya shule. Lakini hakushtaki. Video hiyo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji kadhaa wakisema kuwa mwalimu huyo achukuliwe hatua.

Source:BBC

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.