Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

TAARIFA ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu Mwenendo wa uchumi wa Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema uchumi wa Tanzania unaendelea kumarika na kuna viashiria vya kupungua kwa changamoto za upungufu wa fedha za kigeni Nchini.

“Mwenendo wa uchumi wa Tanzania umekuwa wa kuridhisha ambapo ukuaji wa uchumi ulifikia asilimia 4.7 mwaka 2022 na asilimia 5.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, mfumuko wa bei umeendelea kupungua kufikia asilimia 3.3 mwezi Julai 2023 ukilinganisha na asilimia 4.9 mwezi Desemba 2022”

“Urari wa malipo ya huduma na bidhaa nje ya Nchi ulipungua kufikia asilimia 6.3 ya pato la Taifa ukilinganisha na aslimia 7.3 ya pato la Taifa kwa mwaka unaoishia December 2022, vilevile mwenendo wa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani umekuwa wa kuridhisha kuanzia mwanzoni mwa mwezi Agosti 2023 baada ya Benki Kuu kuchukua hatua mbalimbali na kuanza kwa msimu wa mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya Nchi na utalii”

“Mwenendo huu umedhihirika katika soko la rejareja la fedha za kigeni, ambapo kiwango cha kubadilisha shilingi kwa dola ya Marekani umepungua kufikia shilingi 2,550 kwa dola ya Marekani Kutoka shilingi 2,610 mwezi Juni na Julai 2023 ambapo mwenendo huu wa kuridhisha unatarajia kupunguza changamoto ya upungutu wa dola ya Marekani nchini, hali hii pia inajidhihirisha katika kuimarika kwa nakisi ya urari wa malipo na huduma nje ya Nchi (current account deficit)“ ——— imeeleza taarifa ya BOT.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.