Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali

Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha misingi ya kisiasa, kujenga uwezo kwa wanasiasa vijana, sekta za elimu, afya, utalii, biashara na uwekezaji.

Hayo yamebainishwa mkoani Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Yordenis Despaigne Vera.

“Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba kwa muda mrefu na ushirikiano baina ya mataifa haya umekuwa imara tangu ulipooasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Fidel Castro na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Balozi Mbarouk.

Ameongeza kuwa kwa sasa Cuba imeonesha dhamira ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha misingi ya siasa, kuwajengea uwezo wanasiasa vijana pamoja na sekta nyingine kama vile elimu, afya na utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji.

Kwa upande wake Balozi Yordenis Despaigne Vera amesema Cuba inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania kwa takribani miaka 60.

Amesema Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha misingi ya kisiasa kwa manufaa ya Wananchi wa pande zote mbili.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.