Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tunamsaka aliyezusha tumeongeza Mishahara,Luteni Kanali Gaudentius Gervas

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema taarifa iliyosambazwa na mtandao wa kijamii wa Tanzania Abroad TV (TAT) kwamba Wanajeshi wa ngazi za juu wa JWTZ wameongezewa mshahara ni taarifa ya uzushi na upotoshaji.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema “Taarifa hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limelipwa tarehe 18 Agosti 2023, JWTZ inaujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na upotoshaji kwa Jamii hivyo Watanzania waipuuze kwani ina nia ovu”

“Ukweli ni kwamba hadi leo tarehe 19 Agosti 2023 kwa JWTZ haijafika tarehe ya kulipwa mshahara, aidha hakuna ongezeko lolote la mshahara au malipo yoyote kwa Wanajeshi wa ngazi yoyote wa JWTZ yaliyofanyika tarehe 18 Agosti 2023 kama ilivyotajwa na mtandao huo”

“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji huo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.