Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Uboreshwaji wa Matibabu ya Saratani kwa Watoto

Shirika la Global hope kutoka nchini marekani linalojihusisha na matibabu ya Saratani ya watoto limetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la Kuimarisha matibabu ya Saratani kwa watoto.

Ugeni huu umeongozwa na Dkt. Anne Akullo Mkurugenzi msaidizi , Huduma za Tiba katika Shirika la Global hope kanda,pamoja na viongozi wengine wa shirika hilo.

Pia amefurahishwa na jitihada zinazofanyika latika Hospitali ya Bugando katika uimarishaji na upatikanaji wa huduma za saratani, ikiwemo uwepo wa jengo kubwa linalotoa matibabu jumuishi , uwepo wa vifaa tiba, mashine za miozi na wataalamu waliobobea kutoa huduma hizo.

Sambamba na hayo, Dkt. Fabian Massaga Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amewashukuru viongozi wa Global hope kwa kuweza kuanzisha mashirikiano hayo yenye tija katika kutoa matibabu ya Saratani kwa watoto, pia ameahidi kuendeleza umoja huu katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma stahiki kwa wagonjwa.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.