Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Uchunguzi wa mara kwa mara wa meno (angalau mara moja kwa mwaka) unaweza kuokoa pesa nyingi na Maumivu makali ya JINO

Uchunguzi wa mara kwa mara wa meno (angalau mara moja kwa mwaka) unaweza kuokoa pesa nyingi na maumivu makali ya JINO. (Soma hadi mwisho ili kuokoa angalau garama kidogo kwa huduma ya meno).

MENO

Kwa kawaida Meno yana sehemu(layers) tatu ambazo ni;

  1. enamel ,
  2. dentine
  3. Pamoja na pulp .

(1) Enamel; ni sehemu(layer) ya nje kabsa ya jino,ambayo haina nerves zozote, Hivo hata ukiwa na tundu huwezi kugundua au hisi chochote/dalili zozote kwenye eneo hili,

Wakati unafanya checkup ya Meno ndyo inakuwa rahisi kugundulika kama kukiwa na shida yoyote kwenye eneo hili.

Kwa hatua hii daktari wako wa meno atakushauri kuhusu lishe,vitu vya kula na vitu vya kuepuka kula pamoja na kanuni za usafi wa kinywa,

Moja ya vitu ambavyo unashauriwa kuepuka kula kwa wingi ni pamoja na vitu vyenye Sukari nyingi kama vile keki n.k

Pia unaweza kushauriwa kuziba jino lenye shimo au kufanya filling au fissure sealant kwa ajili ya kujaza meno yenye shida.

(2) Dentine; Hii ni sehemu(layer) ya pili ya jino, Layer hii ina nerves mbali mbali mwishoni,

Endapo ulichelewa kwenda kwa wataalam wa meno na kupata Tiba,baada ya uharibifu(decay) wa layer ya kwanza ya jino kutokea huweza kuendelea mpaka kufikia kwenye sehemu hii ya pili,

Unaweza usihisi maumivu yoyote ya jino kwa mwanzoni,ila wakati uharibifu unakaribia layer ya tatu ya jino utaanza kuhisi maumivu,

na maumivu haya huweza kuwa madogo mpaka maumivu makali sana ya jino kutegemea na jinsi uharibifu(decay) wa jino ulivyokaribu na layer ya tatu ambayo ni pulp.

Tatizo likiwa kwenye hatua za mwanzoni huduma ya kuziba jino bado inawezekana(temporary filling may be done to allow the tooth to heal followed by a permanent filling).

(3) Pulp; hii ni sehemu au layer ya tatu ya jino, Hii ndyo sehemu ambayo nerves zote pamoja na mishipa yote ya damu hupatikana hapa.

Uharibifu wowote au shida yoyote ikitokea kwenye eneo hili huweza kupelekea maumivu makali sana ya Jino,

Hapa ndipo hata ukinywa dawa,maumivu yanaweza kuendelea licha ya kutumia dawa za kutuliza maumivu.

Wataalam wa meno wanaweza kukushauri matibabu yanayohusu Root-canal treatment,

ambapo ina maana tu ya kuua vimelea vya magonjwa kama bacteria ndani ya jino na kulifunga kabisa kutoka kwenye Mizizi kwenda juu.

Baada ya matibabu haya ya kwenye mfereji wa mizizi wa jino(Rootcanal treatment), Jino huwa na mvuto sana kwani meno mengi huwa yanaharibika sana kwa hivyo ni vyema ufuatilie huduma hii ili kulinda jino kwa muda mrefu.

KUTOA JINO, Haya ni matibabu ya mwisho kabsa ikiwa kila kitu kimeshindikana, na hii huweza kufanyika kwa meno yaliyoharibiwa sana.

Kutoa jino sio garama sana, ila garama kubwa inaweza kutumika ikiwa unahitaji jino lingine la kudumu sehemu ambapo umetoa jino, kufanya dental implant inaweza kuwa garama kubwa Sana.

Hivo basi, kwenda kufanya checkup ya meno mara kwa mara huweza kukuepusha na matatizo yote haya, kabla ya meno kushambuliwa na kupata madhara ZAIDI.

Natumaini hii itaokoa pesa na maumivu makali ya jino ambayo unaweza kupata baada ya jino kuanza kushambuliwa.

 Remember sharing is caring ?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.