Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wafamasia Waaswa Kutojihusisha Na Wizi Wa Dawa Hospitalini

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi amewataka wafamasia kuzingatia uaminifu pamoja na weledi katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Prof. Janabi ameyasema hayo wakati wa hafla la kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya nne iliyoandaliwa na Idara ya Famasi MNH ambapo Wafamasia watatu Faraji Chambuso, Seleman Madebe na Scholastica Chimani walitunukiwa vyeti na zawadi.

“Maisha ni mbio ndefu (marathon) na mafanikio ni matokeo ya mchakato wa kitambo fulani, usijaribu kudhani maisha ni mbio ya mita mia kwa kujiingiza kwenye vitendo vya wizi wa dawa, hospitali haitavumilia mtumishi wa aina hii akikamatwa atawajibishwa ipasavyo” amesema Prof. Janabi

Aidha amepongeza idara nzima ya famasi kwa kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo limepelekea kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa na kupunguza foleni kwenye madirisha ya dawa.

Awali akiwasilisha taarifa ya idara hiyo, Mkuu wa Idara Mfamasia. Nelson Njau alisema idara imefanikiwa kuongea upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 98, kupunguza gharama za ununuzi ya dawa ambapo katika kipindi cha miezi kumi imeokoa TZS. 2 BIL. ukililinganisha na vipindi vilivyopita, pamoja na kujifunza matumizi bora ya dawa za saratani jambo ambalo limesaidia kuokoa zaidi ya TZS. 200 Mil.

“Tumeingia mikataba mbalimbali ya mashirikiano ikiwemo mkataba na shirika la Direct Relief na hivi karibuni tunategemea kupokea msaada wa dawa zenye thamani ya TZS. 1 BIL. pamoja na mkataba na TMDA ambao matunda yake yameshaanza kuonekana hasa katika eneo la usalama wa dawa” amesema Mfamasia. Nelson

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.