Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Idadi ya vifo vya tetemeko nchini Morocco vyakaribia 2,500

Idadi ya vifo vya tetemeko nchini Morocco vyakaribia 2,500

Idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi lililoitikisa Morocco imepanda na kufikia karibu watu 2,500 leo Jumatatu.

Vikosi vya uokozi vimeendelea na shughuli ya kuwasaka watu ambao pengine wamekwama kwenye vifusi

Takwimu hizo zimetolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco ambayo pia imearifu kuwa watu wengine 2,480 wamejeruhiwa tangu tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Ritcher lilipoikumba nchi hiyo mnamo Ijumaa usiku.

Hii leo waokoaji kutoka Uhispania, Uingereza na Qatar walijiunga na wenzao wa Morocco kufukua vifusi vya majengo yaliyoporomoka kujaribu kuwatafuta walionusurika.

Misaada nayo imendelea kutumwa kutoka kila pembe ya dunia ikiwemo Umoja wa Ulaya ambao umetangaza kuipatia Morocco kitita cha dola milioni 1 kusaidia juhudi za kuwahudumia walioathirika na janga hilo.

Source:dw_swahili

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.