Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kuna hofu kwamba huenda watu 20,000 wamefariki na mafuriko – Libya

Kuna hofu kwamba huenda watu 20,000 wamefariki katika mafuriko yaliyokumba eneo la mashariki mwa Libya siku ya Jumapili.

Meya wa mji wa bandari ulioharibiwa wa Derna alisema idadi hiyo ilitokana na idadi ya wilaya zilizoathiriwa kabisa wakati mabwawa mawili yalipopasuka, na kutoa tsunami ya maji wakati wa usiku ambapo watu walikuwa wamelala.

Zaidi ya watu 5,300 hadi sasa wamethibitishwa kufariki na wengine takriban 30,000 wakilazimika kuyahama makazi yao kutokana na mafuriko hayo.

Wafanyakazi wa misaada kutoka shirika la usaidizi la matibabu, Médecins Sans Frontières, wanatarajiwa kuwasili jijini leo (Alhamisi), na kujiunga na timu za kukabiliana na dharura.Miili mingi bado haijaopolewa chini ya vifusi au baharini, huku waokoaji wakiomba mifuko zaidi ya mwili.

Maelfu bado hawajulikani walipo huku waokoaji wakihangaika kufika Derna.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.