Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kutoka damu baada ya tendo ni dalili ya Ugonjwa gani?

Kutoka damu baada ya tendo ni dalili ya Ugonjwa gani?

Fahamu kuhusu chanzo cha mwanamke kutoka damu baada ya tendo la ndoa, Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea mwanamke kupata tatizo la kutoka damu baada ya tendo,

Baadhi ya Sababu hizo ni Pamoja na;

1. Mwanamke kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo PID N.k,

Mwanamke Kuwa na magonjwa ya Zinaa kama vile; Ugonjwa wa Pangusa(chlamydia) n.k

2. Mwanamke kuwa na tatizo la Ukavu ukeni-vaginal dryness (atrophic vaginitis)

3. Mwanamke Kuwa na michubuko ukeni,mpasuko au majeraha yoyote,

ambapo mwanamke huweza kupata matatizo haya kwa sababu mbali mbali ikiwemo;

  • kupata mpasuko(tears) wakati wa kujifungua,
  • tatizo la ukavu ukeni
  • au msuguano mkali wakati wa tendo la ndoa. n.k..

4. Kuwa na dalili za tatizo la uvimbe kwenye kizazi,

Mwanamke huweza kutoka damu baada ya tendo la ndoa kama ana matatizo kama haya;

  • cervical/ endometrial polyps
  • cervical ectropion n.k

Miongoni mwa Sababu kubwa za mwanamke kutoka damu baada ya tendo la ndoa ni pamoja na kuwa na tatizo la cervical polyps.

Tatizo hili huhusisha mwanamke kuwa na  ukuaji wa nyama/uvimbe wenye takribani cm 1 mpaka 2, Na mara nyingi hutokea kwenye mlango wa Kizazi(Cervical openning).

5. Na wakati mwingine kutoka damu baada ya tendo huweza kuwa dalili ya Saratani ya shingo ya kizazi au saratani ya ukeni(cervical or vaginal cancer).

6. Tatizo la kutoka damu baada ya tendo la ndoa huweza kusababishwa na kuvimba kwa mlango wa kizazi(cervical inflammation, or cervicitis)

ambapo hali hii huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo magonjwa ya zinaa kama vile;

  • Ugonjwa wa Pangusa(chlamydia)
  • Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea) n.k

7. Sababuzingine ni pamoja na;

– Msuguano mkali wakati wa tendo la ndoa

– Mwanamke kuwa na shida ya Ukavu ukeni

– Kutoka damu ukeni kama umefanya tendo la ndoa karibu na kuanza period au mara tu baada ya kumaliza period

– Kupata maambukizi ukeni au kwenye mlango wa kizazi

– Kupata vidonda ukeni(Genital sores) kwa sababu ya maambukizi ya herpes n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.