Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mchango wa Dini Tunauheshimu ili kuimarisha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii kwa Wananchi

Waziri Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuthamini, kutambua na kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini katika kuimarisha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii kwa Wananchi.

Ameyasema hayo leo Jumapili, Septemba 3, 2023 alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mteule Thomas John Kiangio, Askofu Katoliki wa Jimbo la Tanga iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Antony wa Padua lililopo Chumbageni Jijini Tanga.

Waziri Mkuu ametoa rai kwa Viongozi wa dini, Waumini na Watanzania kwa ujumla wazidishe upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa jamii ya Watanzania kwa sababu asili ya dini ni upendo kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mwanadamu “Hivyo basi, uwepo wa upendo ni msingi mzuri wa kuendelea kulinda amani tuliyonayo katika Taifa letu”

Askofu Thomas John Kiangio alizaliwa tarehe 17 Machi, 1965 katika kijiji cha Mazinde Ngua Wilayani Korogwe, Tanga na anakuwa Aksofu wa tano baada ya kifo cha aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Hayati Askofu Anthony Banzi aliyefariki tarehe 20 Desemba, 2020.

Askofu Kiangio amewahi kushika nafasi za kichungaji katika Parokia ya Ekaristi Takatifu huko Lushoto na pia amehudumu katika nafasi ya Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Tanga kuanzia mwaka 2020 hadi 07 Juni 2023 alipoteuliwa kuwa Askofu Mteule, pia amewahi kutumikia katika nafasi ya Gombera Msaidizi (Rector).

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.