Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

MOUNT MERU imekuwa mshindi kwa mabadiliko ya maendeleo kwa hospitali za rufaa za mikoa

MOUNT MERU imekuwa mshindi kwa mabadiliko ya maendeleo kwa hospitali za rufaa za mikoa

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru leo Septemba 14, 2023 wakabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza wa hospitali za Rufaa za Mikoa wa mabadiliko ya maendeleo yanayoonekana kwenye miundo mbinu, vifaa tiba pamoja na utoaji wa huduma bora za Afya katika kikao kazi cha Waganga Wafawidhi na viongozi wa hospitali za Rufaa za Mikoa kilichofanyika kuanzia Septemba 11 hadi 14, 2023 Jijini Arusha.

Akifunga kikao kazi hicho aliekuwa mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewapongeza Viongozi hao kwa kujitoa kwao kwenye huduma za Afya kwa kushirikiana na ngazi za hospitali za Wilaya na kata lakini pia kuweza kupata fursa hii ya kukaa kwa pamoja na kujitathimini kwa kazi zilizofanyika kwa kupima malengo waliojiwekeza na mahali walipofikia na pia kutizama mipango ijayo ya bajeti inayokuja ya mwaka wa fedha 2023/2024 na kuweka mikakati ya jinsi ya kutekeleza majukumu na malengo ya mwaka huu wa fedha wa 2022/2023.

Aidha amesisitiza katika huduma kwa wateja (Customer Service) ili kuweza kufanikisha utoaji wa huduma bora za Afya kwa Wateja na kueleza kuna kazi kubwa ya kuwajengea uwezo Watumishi wa ngazi za chini ili kufanikisha mawasiliano bora baina ya watumishi wa Afya na wateja wao lakini pia aligusia katika uboreshaji wa utumiaji wa mifumo ya utoaji huduma katika kuimarisha usimamizi ili kupunguza upoteaji wa vifaa tiba, dawa na changamoto zitokanazo na madai ya bima za Afya swala litakalo saidia kuongezeka kwa mapato.

Vilevile amempongeza Mganga Mfawidhi wa Mount Meru Dkt. Alex Ernest kwa kufanikisha utoaji huduma bora na kufanya hospitali ya Rufaa ya Mkoa kuwa kimbilio kwa Wananchi na wageni kwenda kupata huduma za Afya katika Mkoa wa Arusha na Mikoa jirani.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.