Mtoto wa miezi 10 afanyiwa upasuaji wa kuondoa KIJUSI tumboni
Tulikuwa tunatafuta uvimbe kwenye tumbo la mtoto ambaye amekuwa akilia kwa maumivu kwa miezi kadhaa.
Hata hivyo, tulishangaa kuona vidole vya miguu kwenye tumbo lake, hatukuelewa ni nini,”
Daktari wa upasuaji, Dokta Mushtaq anasema kilichomo tumboni mwa Shazia ni kijusi cha pacha wake. Kijusi kilichoacha kukua katika wiki ya nane au tisa.
“Tuliona umbo la miguu na mikono. Hata vidole. Macho yako nusu,” Mushtaq anasema.
Upasuaji huo ulifanyika katika Hospitali ya Sheikh Zayed huko Rahim Yarkhan, Punjab, Pakistan.
Hiki ni kijusi tumboni mwa mtoto. Hali hii hutokea katika hatua za mwanzo za maendeleo ya kijusi. Pale kiinitete kimoja kinapofunikwa na kiinitete kingine.
Kiinitete cha ndani hakikui vizuri. Kinategemea kiinitete kikuu kwa ajili ya kuishi. Lakini, mapacha wa aina hiyo kawaida hufariki dunia wakati wa kuzaliwa.