Muswada wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia Moja kifungo miaka 50 – Kenya
Muswada unaopendekezwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya unataka watu wa mapenzi ya jinsia moja kufungwa jela miaka 50 kwa kufanya mapenzi bila ridhaa.
Unaitwa Muswada wa Ulinzi wa Familia wa 2023, rasimu ya sheria inayofadhiliwa na mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma, unapendekeza kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja, miungano ya watu wa jinsia moja na shughuli na kampeni zozote za LGBTQ.
Pia unalenga kupiga marufuku maandamano ya watu wa mapenzi ya jinsia moja, mikusanyiko na maandamano barabarani, na mavazi ya yanayoashiria kuwa mpenzi wa jinsia moja hadharani.
“Mtu anayeshiriki tendo la ndoa na mtu wa jinsia moja bila ridhaa ya mtu mwingine akapatikana na hatia atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 10 na kisichozidi miaka 50,” unasema muswada huo.