Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

paul Kagame ana mpango wa kugombea kwa awamu ya nne uchaguzi 2024

paul Kagame kwa mara ya kwanza amesema ana mpango wa kugombea kwa awamu ya nne uchaguzi uliopangwa kufanyika mwakani.

Kagame aliyetawala taifa hilo kwa mkono wa chuma na kwa miongo kadhaa ameliambia gazeti la lugha ya kifaransa la Jeune Afrique kuhusiana na nia yake hiyo katika mahojiano yaliyochapishwa mitandaoni jana Jumanne.

Amesema anafurahishwa na imani waliyonayo watu wa Rwanda juu yake na kuahidi kuwatumikia siku zote na kwa namna atakavyoweza.

Kagame hajawahi kuweka wazi nia ya kuwania tena urais, lakini mabadiliko tata ya katiba yalimfungulia njia ya kuwania awamu ya tatu na kushinda kwa asilimia 99 katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2017.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.