Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Serikali kwa kushirikiana na Wadau Kuimarisha Huduma za Uchunguzi wa Maabara

Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kushirikiana na wadau wa huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa kuimarisha huduma za uchunguzi wa maabara, Vifaa-Tiba, damu salama pamoja na ubora wa huduma ili kutekeleza maelekezo ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi Dkt. Alex Magesa wakati akifungua mkutano wa kitengo cha huduma za uchunguzi wa magonjwa pamoja na wadau wa huduma za uchunguzi wa magonjwa kilichofanyika Jijini Dodoma.

“Tunaendelea kushirikiana na wadau hawa ili kuondoa kero kwa wananchi, ambapo miongoni mwa kero hizo ni pamoja na upatikanaji wa Vitendanishi, Vifaa, Vifaa-Tiba ikiwemo ya mionzi na upande wa damu salama”, amesema Dkt. Magesa

Vile vile, Dkt. Magesa amesema mkazo unawekwa katika kuimarisha upatikanaji wa wataalamu wa maabara, radiolojia, na fundi sanifu vifaa tiba na kuwasisitiza wadau kutoa kipaumbele kwa ajira za muda mfupi kwa wataalamu wa kada husika.

Amesema, ili kufanikisha hayo lazima kazi ifanyike Kama timu ambapo kikao hicho kikimalizika wajumbe wataondoka na maazimio ambayo yatawezesha kwa kila mmoja kujua majukumu yake na anasaidiaje katika kufikia malengo makuu ya Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla.

“Lengo la mkutano huo ni kuwasiliana na kujadili vipaumbele vya huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa wadau wote ili kuweka mikakati ya pamoja ya kufikia malengo ya Wizara ya Afya katika kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa”. Amesema Dkt. Magesa.

Aidha, Dkt. Magesa amesema, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alitoa malengo mbalimbali ambayo yanatakiwa kutekelezwa kwa wakati ili kutatua kero za wananchi ndio maana wameamua kuitisha nguvu ya pamoja ikiwemo nguvu za wadau.

Pia, amesema kwenye mashirikiano hayo yatawezesha kusongesha gurudumu la maendeleo katika upande wa uchunguzi na kutoa huduma zilizo bora ili kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.