Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Vijana Mtoke Vijiweni Mfwate Ajira Shambani

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Ng’waniduhu Malenya amewataka Wananchi hususani Vijana kutokaa vijiweni wakilalamika kuwa hakuna ajira na maisha magumu na badala yake wajiongeze kwa kujishughulisha na kilimo ambacho amesema kinalipa na wapo waliotajirika kupitia kilimo huku akisema Wilaya hiyo imepanga kufanya mapinduzi ya kilimo.

DC Ngollo @ngollomidalla amesema ili kuwafanya Wananchi washawishike kulima amenunua na kugawa bure majembe 500 kwa Wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua Sekta ya Kilimo nchini.

“Tunataka tufanye mapinduzi ya kilimo, Mh.Rais August 08,2023 alitangaza Mkoa wa Ruvuma kuwa tunaongoza kwa uzalishaji kwahiyo Mkoa wa Ruvuma ni Baba lao kwa uzalishaji wa chakula na Namtumbo tukiwemo”

Malenya ametoa majembe hayo wakati wa Kilele cha Jukwaa la Utambuzi wa Fursa za Kilimo, Biashara na Utalii (Namtumbo Kihenge) lililofanyika Namtumbo na kuhudhuria na Wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, pia Benki ya NMB @nmbtanzania ni miongoni mwa Wadau walioshiriki, Wadau wengine ni TFS, TIC, ASA, Nyerere National Park, Mantra Tanzania Rosatom na SONAMCU.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.